Tukakaa mpaka saa nne kasoro asubuhi Bakari kimwanga, wa gazet Mtanzania akapewa simu aongee na Badra Masoud, juu ya nini kinaendelea. Akaambiwa kazi ni kubwa wafanye subra...
Waandishi wakakasirika wakaamua kutoka nje kuenda kuangalia shughuli zao. Maana kazi ni nyingi mjini.
Wapo ambao waliamua kubaki, na kwa kuwa Tanesco hakuna sehemu za kukaa wengine walikaa hata sehemu zisizopasa kukaliwa. Ilikuwa balaaa..
Akaanza kuwaeleza tukio zima kuwa kuna wakorofi wanaliibia taifa tuende tukawakamate. Ila kwanza lazime wakajipange na viongozi wake. Tukaambiwa tusubiri.
Hata kamanda wa matukio "Mwaikenda wa gazeti Jambo Leo na mmiliki wa blogu ya 'kamanda wa matukio' pia alikuwepo.
No comments:
Post a Comment