Ndugu zangu,
Mnakumbuka siku mbili
zilizopita niliwaahidi kuwapa habari njema. Naam kutimiza ahadi ni moja ya
mambo ninayoyaheshimu sana
katika dunia hii, maana hunifanya kuwa mwaminifu na huniongezea marafiki wengi
kupita kiasi.
Haya, mtakumbuka tulianza
pamoja kuitangaza blogu hii ya ‘kidojembe’ na namshukuru Mungu tangu tumeanza
zoezi hilo sasa
ni miezi miwli, maana ilikuwa ni mwezi june 28 mwaka huu. Na sasa imefikisha
wadau 10250 na hutembelewa na wastani wa wadau 500 mpaka 600 kwa siku ambalo ni
fanikio la hali ya juu na hata sikutegemea hali hiyo. Nchi inazozitebelea ni:- USA ,UK ,
Russia , Tanzania , Kenya ,
Uganda , UAE, Belgium , Oman ,
Canada , Netherlands , Denmark , German.
Lakini kuna tatizo; nahitaji
kuipanga blogu hii na kuiweka katika muonekano unaofaa na kusomeka kwa urahisi.
Kazi hizi hufanywa na watu maalum kwa malipo yanoyofanana na kazi. Hivyo
nahitaji kufanya hivyo haraka iwezekanavyo. Maana wapo wadau wameshaanza
kunilalamikia kuwa blogu yangu haikidhi viwango na si ‘readers friendly’ si tusi
bali ni ushauri wa kitaalamu. Kwa sisi wanahabari tumejifunza kitu kizuri sana . Maana msomaji
hatakiwi kujaziwa kila kitu katika ukurasa mmoja, lazima macho yapumbazwe na
picha ama vitu vinavyotembea (animation).
Kitu kinachonikwaza ni kuwa mpaka sasa
sijampata mtu mahiri ambae anaweza kuitengeneza blogu hii na kuweza kusomeka.
Ili hata wale watakaotaka kuleta matangazo yao basi yapate sehemu nzuri na yaonekane
vema.
Natangaza biashara na watu
wanaotengeneza ama kusanifu kurasa za blogu, kama
kuna mtu anamfahamu msanifu blogu basi anipe mawasiliano yake ama awasiliane na
mimi kwa namba ama barua pepe hapo chini.
Kadhalika naalika watu wenye
matangazo yao ,
nitawatolea bure matangazo ambayo hayatahitaji kusanifiwa ama kuwekwa katika
mtiririka wa kupanda ama kushuka (animation) matangazo hayo nitayatoa bure….
Nasema tena bure. Hivyo wakati wako ni huu, wasiliana nami kwa namba hizo chini
na uweke picha za bidhaa zako usisahau kuweka mawasiliano ya kutosha ili kuweza
kuwafanya wateja kukupata kirahisi.
Sifanyi hivi kwa kutaka sifa,
bali ni shukurani kwa wadau wangu ambao ndani ya miezi miwili wamekuwa wengi
kiasi cha kunipa raha. Watu zaidi ya 10,000 si mchezo. Nimepata kuona blogu
ambazo zina miaka miwili mpaka mitatu lakini hazijafikia idadi hiyo ya wadau.
Tena ni blogu zilizosanifiwa na zinapendeza kwelikweli.
Ahsanteni,
HAFIDH ATHUMANI ABDALLAH KIDO
AL-BAAJUN
KIJITONYAMA ALIMAUA ‘B’ DAR
ES SALAAM , TANZANIA
0713 593894/ 0752 593894
3/08/2012
No comments:
Post a Comment