Jaji mmoja nchini Ufaransa amewaomba polisi wa Uingereza
wamkamate kiongozi wa ujumbe wa Olimpik wa Morocco
ambaye kwa sasa yuko jijini London .
Kiongozi huyo wa Olimpiki Jenerali Housni Benslimane,anadaiwa
kuhusika na kutoweka kwa kiongozi wa upinzani wa Morocco Bwana Mehdi Ben Barka.
Mwanasiasa huyo wa upinzani wa Morocco
wa alitoweka mwaka 1965 akiwa Ufaransa.
Jaji
Patrick Ramael tangu mwaka wa 2007 amekuwa akitaka Housni Benslimane akamatwe.
Jaji
huyo amekuwa akitaka kiongozi huyo wa Olimpik na wanajeshi watatu wa zamani wa Morocco wahijiwe kutokana na kutekwa nyara kwa
Bwana Ben Barka mjini Paris .
Lakini
ubalozi wa Moroccan mjini London
unasema kuwa Jenerali Benslimane alikuwa jijini humo wiki iliyopita lakini
ameshaondoka.
Ingawa
Jaji Ramael alitoa waranta yakutaka kiongozi huyo wa Olimpiki akamatwe miaka
saba iliyopia lakini haitambuliki kwa sababu hadi sasa polisi wa kimataifa
Iterpol na wakuu wa mashitaka nchini Ufaransa bado hawajaikubali.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment