Wednesday, August 8, 2012

Leo ni sikukuu jamani.... Nilipiga picha namna siku yangu ilivyokuwa tangu asubuhi mpaka alasiri.... Uvivu kwa kuenda mbele....

 Niliamka nikaona kiwingu na mvua za rasharasha, nikajua ni sikukuu lakini kwa kuwa leo gazeti Raia Mwema ndiyo linatoka nikasema wacha tu niende ofisini nikakae nisogeze dakika.

 Kama kawaida nlipopita pale kwa mateja nikakuta bado wamelala kibarazani huku wanauzamaji kwa kukata mabomba. Dawasco hata sijui kwanini hawatembelei kidojembe wawaone hawa jamaa wanavyoharibu miundombinu ya maji. Mpaka wakazi wa Tandale wanapata tabu ya maji kama hawapo mjini.

 Hiki ni kituo cha daladala cha Tandale Shule, yaani kilikuwa kitupuuu, wakati kinaajaa watu balaa...

 Kufika shekilango mvua ilikuwa inanyesha balaaa, mpaka ikabidi nikimbie maana ukifanya mchezo unazifua nguo hali zikiwa mwilini.

                                               Mvua ilikuwa kubwa wadau

Kufika ofisini hakukuwa na mtu, ila watu wa usambazaji, nikasoma magazeti ya leo harakaharaka  halafunikachukua nakala yangu ya Raia mwema juu ya meza nikaondoka.

 Katika baadhi ya magazeti picha hizi ndizo zilizonivutia,moja ilikuwa ni ya Juma Kaseja kubeba mtoto aliepewa jina lake.

Ya pili ni hii ya enzi za Mwalimu na Karume.

 Niliporudi nyumbani nikafikia kitandani mja kwa mojampaka saa sita mchana mvua ilipoacha kunyesha.

Mpaka kwenye saa tisa alasiri hivi ndipo jua likaanza kuchomoza, ndipo nikajua kweli mji huu noma...

No comments:

Post a Comment