Mtoto wa Kanali Gaddafi amesema anataka kesi yake
iendeshwe The Hague, badala ya kuendeshwa nchini Libya, mawakili wake wamesema.
Saif al-Islam alisema iwapo kesi yake itaendeshwa Libya basi
inakuwa sawa na kuuawa, kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa mahakama ya ICC.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 40
anashikiliwa na wapiganaji mjini Zintan. Amekuwa akishikiliwa Libya tangu
Novemba 2011
Alishtakiwa
na ICC kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Serikali
ya mpito ya Libya mpaka sasa
imekataa kumkabidhi Saif Uholanzi ambako mahakama ya ICC iko ikisema kuwa hana
budi kukabiliana na mashataka yake nchini Libya .
Kanali
Gaddafi, ambaye utawala wake wa kidikteta ulidumu kwa miaka 42 aliuawa katika
mazingira ya kutatanisha baada ya kukamatwa na waasi mwezi Octoba, katika
kitendo ambacho kilishutumiwa vikali na makundi ya haki za binadamu.
'Ulinzi
wa bandia'
"Siogopi
kufa lakini ikiwa itaendeshwa hapa hiyo muuite tu kuwa ni uuaji na
mmalizane," Saif al-Islam alinukuliwa na mawakili akisema.
Mwezi
Juni, wafanyakazi waliotumwa na ICC walikamatwa baada ya kukutana na Saif
al-Islam, na kushikiliwa kwa zaidi ya wiki tatu.
Nyaraka
zilizowasilishwa mahakamani zinasema wakati wa mkutano huo afisa aliyejifanya
mlinzi alimzuia mwanasheria wa ICC kuchukua kiapo kutoka kwa Saif al-Islam.
"Mlinzi
huyo ambaye kimsingi ni Bw Ahmed Amer – mwanasheria anayezungumza lugha kadhaa
alijumuishwa kwenye timu hiyo makusudi kuwalaghai " nyaraka ziliandika,
kwa mujibu wa Reuters.
"Alirejea
chumbani na (mkalimani wa ICC akiwepo) alianza kupiga kelele kuwa maelezo hayo
yalikuwa hatari sana , yamekiuka usalama wa Libya na kwa
Ulinzi wasingeyarudisha"
Mkutano
ulistishwa baada ya dakika 45 na nyaraka zao kuharibiwa, wakili alisema.
Baadaye walikamatwa.
Hatua
hiyo ilionekana kuwa "kimyume cha sharia, uhaini na ukiukwaji wa taratibu
za usalama wa Taifa kwa ama Bw Gaddafi au washauri wake na kuonyesha kuwa
Gaddafi hataki kesi yake iendeshwe na mahakama za Libya ." Walisema mawakili
kwenye nyaraka.
Maafisa
wa Libya
walimshutumu wakili Melinda Taylor, aliyekuwa akiongoza ujumbe wa ICC, kwa kuwa
na vifaa vya upelelezi vikiwa vimeshikizwa kwenye barua ya Saif al-Islam wakati
wa mkutano.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment