Ajali ya
basi ya Tony Sley yenye namba za
usajili T 218 ACH lililokuwa
likitokea Tunduma mkoani Mbeya
kwenda jijiniD’Salaam imeua watu watatu wakiwemo wawili raia ya Zambia na mmoja mtanzania na
kujeruhi wengine 38.
Ajali hiyo imetokea
katika eneo la kona za mlima wa
kitonga kwenye barabara kuu ya
Iringa –D’Salaam jana majira
yasaa 12 za jioni baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulipita lori lilolokuwa
mbele yake.
Wakizungumza
katika eneo hilo na Hospitali ya mkoa wa Iringa majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa
katika hospitali yawilaya ya Kilolo Ilula walisema kuwa chanzo cha ajali
hiyo ni uzembe wa dereva wao alisema Agnes Lukasi (30).
Agnesy alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amekaa siti ya mbele na wakati dereva huyo akifanya uzembe huyowalikuwa wakimshuhudia hata kujaribu kumuonya bila mafanikio.
Alisema kuwa katika basi hilo alikuwa na mtoto wake Dina Lukas (4) ambaye pia amejeruhiwa katika paji lake la uso.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamhanda ambaye alifika eneo la tukio pamoja na mkuu wa kikosi chausalama barabarani mkoa wa Iringa aliuthibitishia mtandao huu kuwa jumla ya abiria
38 ndio waliojeruhiwa katika ajalihiyo.
Aliwataja baadhi ya majeruhi ambao majina yao yamepatikana
na kulazwa katika hospital teuli ya mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja na Boyd Simwings(43) ,
Violet Chambale(35),Zilombo Wake(38),Warmen Mambwe (33),Eugen Maluge(39),
Mwamba Andrew (27) , Bright Mwalukanga (33) na John Lemba( 30) wote raia wa Zambia.
Wengine ni Martine Shombe( 29) mkazi wa Tunduma, Zainabu Amuri (32) mkazi wa D’Salaam , Efrain Mwampashi (31)
mkazi wa Tunduma, Sebastian Mhaya(25) mkazi wa
Tunduma, Vedastus Benjamin (11)
mkazi wa Tunduma, Mrashi Handu
(38) mkazi wa Igulusi, Juma
Ramadhan (40) mkazi wa Tunduma, Twaribu Juhim (39) mkazi wa Arusha, Muka Muka
(26) mkazi wa Tunduma, Edina Ramadhan (3) mkazi wa Tunduma
na Benjamin Enock (33) mkazi wa
Mbeya.
Wengine ni Agness
Lukas (30) mkazi wa Tunduma , Dina Lukas (4) mkazi wa Tunduma
Beatrice Msakanti( 42) mkazi wa Zambia, Besa Shadrack (32) mkazi wa Zambia na Mary Mumba (48) mkazi wa Zambia pia.
Alisema majina ya majeruhi zaidi yatapatikana hivi karibuni baada ya majeruhi waliopo Hospital ya wilaya ya Kilolo Ilula kufika mjini Iringa.
Mbali ya majeruhi hao pia aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Cla Pily (32) na Dany Kawina (43)
wotewafanyabiashara raia wa Zambia pamoja na Abel Nelson (32) ambaye ni
mtanzania.
Kamanda Kamhanda mbali ya kueleza masikitiko yake juu ya ajali hiyo bado aliwaonya madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuendesha kwa uangalifu wa hali ya juu na kuwa jeshi lake mkoani Iringa halitalala kuwabana madereva wazembe.
Chanzo: www.francisgodwin.blogspot.com
No comments:
Post a Comment