Tuesday, July 24, 2012

Kamera yetu mtaani leo.....

 Mtaani kwetu magari hakuna na ndiyo maana tunachota maji katikati ya barabara bila ya wasiwasi wowote..

 Hawa ni watoto hawazidi hata umri wa miaka sita, wanaombaomba mitaa ya mjini. Wazazi wao hawawajali je Serikalipia haiwajali? Wanawakimbiza wamachinga ambao wanatafuta riziki je hawa mnawafanyaje?

                      Huyu dada nae ni muandishi anatafuta Press Card bila mafanikio Maelezo humu.

                    Idara hii iwe makini kutoa majibu kwa wanahabari wanaotaka Press Card.

 Kama kawaida yangu nikikutana na wewe mtu wangu wa karibu ambae tumepotezana siku nyingi lazima nipate kumbukumbu yako. Wa katikati anaitwa Thabeet Likokola, ni mwajiriwa wa wizara ya fedha kitengo cha teknohama (ICT), nilikuwa nae Times School of Journalism wakati tunagonga Diploma ya uandishi. Wa mwanzo kulia anaitwa Tiganya Misenyi, ni mwajiriwa wa Wizara ya Habari yupo MAELEZO nilimuuliza kama Press Card nitapata akabaki anacheka hakuwa na majibu mwafaka hatari hii....

 Hapa ni Kisutu, zamani ndipo palipokuwa na kituo cha mabasi yanayokwenda mikoani mnapakumbuka wadau wa Mbeya, Moshi na Arusha?

 Huyu anaitwa Feisal Abdu, ni muoga wa kupigwa picha hapa alikuwa ananiambia 'sitaki kuwekwa facebook' jembe hili la masuala ya simu za mkononi mtaalamu sana wa kutengeneza vifaa ya elektroniki. Nilikuwa nae kidato cha kwanza mwaka 1999 Masjid Qubah Seminary School..... Sinza Mori. Nilipotezana nae kwa takriban mwaka na nusu sasa..

 Matunfda haya ni mazuri sana kwa wanaofunga, maana mwili wa mwanadamu unahitaji maji mengi, hivyo ukifuturu jitahidi unapata japo kipande.

No comments:

Post a Comment