Monday, July 23, 2012

Futari ya leo...

Ndugu zangu,

Leo tena nawaletea futari mwanana ambayo itakusaidia kukujengea afya na kukuacha na shibe ambayo haina   madhara kwa mwili wako. Kadhalika siku ya pili hautokuwa na uchovu wa kupita kiasi ambao utawafanya watu wanaopinga funga waseme kufunga ni mateso.

Leo tutapika ndizi mbichi za nazi zilizochanganywa na nyama ama samaki. Halafu tuweke vibibi kwa wale wanaovijua, tena tutawekana maandazi (maamri), halafu tutamalizia na mkate wa boflo (loaf). Usisahau maziwa matupu yasiyo na sukari wala majani ya chai (tea leafs).

Katika matunda leo tutaweka tikiti maji (water melon), ndizi mbivu (yellow banana) na machungwa. Usiache unywa maji mengi baada ya saa moja ya kufuturu.

Ramadhan Kareem.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
24/07/2012

No comments:

Post a Comment