Monday, July 23, 2012

Athumani Iddy Chuji aiingiza Yanga Nusu Fainali Kombe la kagame leo dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar....



Leo mchezaji wa timu ya Yanga Athumani Iddy Chuji ameiwezesha klabu yake kuingia hatu aya nusu fainali baada ya kumalizia penati ya mwisho na kufanya kuwa penati tano kwa tatu dhidi ya klabu ya Mafunzo kutoka Zanzibar.

Awali katika dakika arobaini za mwanzo timu ya mafunzo ilionekana kuwa na uhai sana hasa baada ya Ali Mmanga kuipatia bao la kwanza klabu yake ya mafunzo na kuifanya Yanga kurudi mapumziko ikiwa kichwa chini.

Lakini wakati wa kipindi cha pili dakika ya mwanzo Said Mhanuzi aliiondolea unyonge klabu yake ya Yanga kwa kusawazisha na kufanya vibao vya magoli kusomeka mojamoja.

Hali hiyo ilifanya kuingia hatua ya matuta baada ya dakika tisini za kawaida kuisha, na matokeoya penalt yalikuwa ni 3 kwa 5 baada ya mchezajimmoja wa mafunzokukosa penalt.

No comments:

Post a Comment