Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene IsakaMamlaka ya Usimamizi na
Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema kuanzia sasa mwanachama
wa mfuko wowote hataruhusiwa kuchukua mafao yake kutokana na sababu yoyote
mpaka hapo atakapofikisha miaka 55.
Hata hivyo, licha ya kuzuia fao la kujitoa na kutoruhusiwa kuchukua mafaoyao ,
mwanachama wakiwamo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Pensheni ya
Mashirika ya Umma NSSF) atapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia
dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa
kwenye sheria ya SSRA.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, mabadiliko hayo yametokana na sheria za mamlaka hiyo kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge Aprili 13, mwaka huu na kwamba imeshasainiwa na Rais Jakaya Kikwete na imeanza kutumika rasmi.
Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo.
“Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi lakini kuanzia sasa mwanachama wa mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (55) au kwa lazima (60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu” ilisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kufafanua kuwa:
“Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni.
Taarifa ya Mkurugenzi huyo iliendelea kusema kuwa mafao ya kujitoa yanapunguza na kuondoa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.
Hata hivyo, ilisema pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya madini yataendelea kutolewakama kawaida ikiwemo kuumia kazini
pamoja na fao la ulemavu.
Ilisema wanachama wanatakiwa kuwa watulivu kuhusiana na mabadiliko hayo na kwamba maslahiyao yatalindwa na hakuna atakayepunjwa
kutokana na utaratibu huo.
CHANZO: NIPASHE
Hata hivyo, licha ya kuzuia fao la kujitoa na kutoruhusiwa kuchukua mafao
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, mabadiliko hayo yametokana na sheria za mamlaka hiyo kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge Aprili 13, mwaka huu na kwamba imeshasainiwa na Rais Jakaya Kikwete na imeanza kutumika rasmi.
Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo.
“Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi lakini kuanzia sasa mwanachama wa mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (55) au kwa lazima (60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu” ilisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kufafanua kuwa:
“Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni.
Taarifa ya Mkurugenzi huyo iliendelea kusema kuwa mafao ya kujitoa yanapunguza na kuondoa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.
Hata hivyo, ilisema pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya madini yataendelea kutolewa
Ilisema wanachama wanatakiwa kuwa watulivu kuhusiana na mabadiliko hayo na kwamba maslahi
CHANZO: NIPASHE
vingoz tumie busara katika kutoa maamuz tunajua mn elimu,inakuaje maamuzi yenu mnayatoa kama mtu wa darasa la saba? hasa sekta binafsi ajira zake soi za kudumu tofauti na serikalini, tumieni busara katika kuamua jambo sio kukurupuka tu muogopeni Mungu wanaoumia ni
ReplyDeletewananchi wa hali ya chini hususan WALINZI utamwmbia vp mtu kama huu alinde hadi 55yrs??? kweli huo ndo busara?????? wahusika hizo ni haki za watu aacheni kuleta sera kama mnaongoza familia zenu
ReplyDeleteRAISI JOHN POMBE MAGUFULI we ndo kimbilio letu we najua mtetezi wa wanyonge aangalia PPF kuna nn?????????????????? kwa kweli hawana utu hata kidogo
ReplyDelete