Benjamin Masese, mwandishi wa gazeti la Mtanzania akitetea wananchi katika kituo cha mabasi Manyanya, leo mchana.
Ndugu zangu
Waandishi wa habari ni watu ambao tunapaswa kutetea haki za wanyonge, leo wakati tulipokuwa tunatoka ofisi za CHADEMA mtaa wa Ufipa tulikutana na kituko hiki. Nikiwa na jembe langu Masese wa Mtanzania tulikuta wafanyabiashara wakiwa wanatumia kituo cha daladala kuweka vibanda vyao kinyume na taratibu.
Wakati tukilumbana nao hao wafanyabiashara, mpiga picha wa New Habari Deus Mhagale, akatupiga Picha, lakini tukio hilo la kupiga picha nalo likazua utata. Wapo watu ambao walikuwa wakisubiri daladala wakakasirika kwa kitendo hicho cha kupigwa picha bila ya ridhaa yao.
Bila ya kufahamu kuwa tulikuwa tukitetea haki yao ya kupokonywa kituo chao ambapo badala ya kukaa juani wangeweza kukaa kivulini wakisubiri daladala.
HAFIDH KIDO
0713 593894/ 0752 593894
DAR ES SALAAM, TANZANIA.


No comments:
Post a Comment