Hapa akifafanua jambo juu ya matamshi ya dharau ya Serikali.
Akizungumza na makamanda wake baada ya kumalizana na wanahabari..
wanahabari wakifuatilia kwa makini maneno ya katibu mkuu wa chadema makao makuu ya chama hicho leo mchana.
Na Hafidh Kido
Chama cha demokrasia na
maendeleo (CHADEMA), kimetoa tamko la kulaani kitendo cha Serikali kupitia
waziri wa mambo ya ndani na Katibu mkuu mtendaji Ikulu, kusema taarifa za
viongozi wa chama hicho kutishiwa maisha yao
ni kujitafutia umaarufu.
Akizungumza na waandishi wa
habri katika ofisi za makao makuu ya chama hicho katibu mkuu wa CHADEMA Dk
Wilbrod Slaa, amesema chama chao ni chama makini na hakitafuti umaarufu wa
kisiasa kwani ikiwa wanataka umaarufu wataupata kupitia shughuli zao wanazozifanya
katika kulitetea taifa.
“Wapo watu kama
Ombeni Sefue na Dk Emmanuel Nchimbi, wanasema tunajitafutia umaarufu kwa
lipi….” Alihoji na kuenedelea “Kazi ya serikali baada ya kupata taarifa ni
kuchunguza na si kuhoji. Kitengo cha usalama wa taifa kinapata mamilioni ya
pesa wakati wa bajeti kazi yake ni nini?,” alihoji Dk Slaa.
Mbali ya kutoa dukuduku hilo pia CHADEMA kimetoa
mambo manne waliyozungumza jana katika kikao cha dharura cha kamati kuu
kilichokutana jana eneo la Mbezi Garden kuwa ni kufanya awamu nyingine ya ziara
za mikoani baada ya kumalizika kwa operesheni sangara.
“Sisi si chama cha msimu,
tunahakikisha tunatembelea kila eneo ili kutetea maslahi ya mtanzania wa
kawaida, awamu ya pili ya operesheni sangara tulimaliza robo tatu ya nchi nzima
na sasa tumepanga kufika katika mikoa mitano Singida, Dodoma , Morogoro, Iringa na Manyara,”
alisema.
Aidha katika kuhakikisha
wananchi wa hali ya chini wanafikiwa Dk Slaa amesema watatumia siku 44
kutembelea majimbo 44, kata 806 na vijiji 4000 vya mikoa hiyo mitano.
“Katika maeneo yote hayo
tutapiga kelele na kupinga upotoshwaji wa kiharakati kama
unaofanywa na Waziri mkuu Mizengo Pinda ambae akili zake zimeganda. CHADEMA
siyo chama cha msimu kama vilivyo vyama
vingine vinavyosubiri uchaguzi tu.
“Sisi tunadai ‘change’ yetu
ya Rada, Meremeta, Tan Gold, Deep Green na miradi mingine ya kifisadi. Kamwe
hatutanyamaza bali tutaendelea kupiga kelele mpaka kieleweke. Na kauli mbiu
mpya ya operesheni hii ni hakuna kula, kunywa wala kulala mpaka kieleweke,” Dk
slaa.
Mambo mengine ambayo
yaliazimiwa jana katika kikao maalum cha kamati kuu ni kuanzisha anuni ya
kupinga rushwa ndani na nje ya chama, kupima uwajibikaji wa wabunge wa chama
hicho mpaka madiwani na wenyeviti wa vijiji na serikali za mitaa. Kadhalika wataliangalia
kwa undani sualala kukusanya maoni ya mabadiliko ya katiba ili kuhakikisha
hakuna upotoshwaji kama ilivyokuwa katika
kamati ya wali ya jaji Kisanga.
Siku ya juzi viongozi wa
CHADEMA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, waliitisha
mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho kuzungumzia tatizo la
viongozi wa chama hicho John Mnyika, mbunge wa Ubungo na Dk Slaa katibu mkuu wa
chama hicho.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizotolewa juzi ni kuwa wapo watu ambao walitumwa mjini Dodoma kuchunguza nyendo za Mnyika ili kujua
anapolala, anapokula na anapotembea.
Lakini cha kushangaza
viongozi wa serikali wakiongozwa na Waziri wa mambo ya ndani Dk Nchimbi kuwa
viongozi hao wa CHADEMA si kweli kuwa wanafuatiliwa maisha yao badala yake wanatafuta umaarufu wa
kisiasa.
HAFIDH KIDO
0713 593894/ 0752 593894
DAR ES SALAAM , TANZANIA .




No comments:
Post a Comment