Namshukuru
Mungu mambo yanazidi kuniendea vizuri katika shughuli yangu hii ya blogu. Ni ndoto
yangu ya muda mrefu kumiliki blogu yenye habari mchanganyiko. Kawaida sipendi
kilema cha habari (kuegemea mrengo mmoja).
Nilianza
kama utani tu mwezi uliopita, kwa sasa nina mwezi mmoja na siku chache tangu
nianze kutuma habari yangu ya kwanza katika blogu hii ya kijamii.
Nilianza
na wastani wa watu 15 kwa siku, lakini mpaka ninavyozungumza leo tarehe 12
july, 2012 Alhamisi saa nne na nusu asubuhi (10:30am) nilikuwa na watu 104.
zingatia si watembeleaji wa wakati wote, bali tangu siku ya leo ianze asubuhi
mpaka saa nne blogu yangu imetembelewa na wadau 104 'wakati awali nilikuwa na watembeleaji 15 kwa siku nzima'.
Hivi
ninavyoandika tangu asubuhi mpaka saa sita na nusu mchana nimeshatembelewa na
wadau ‘157 ‘ ambapo ni ongezeko la
wastani wa wadau ‘53‘ ambayo ni ongezeko la asilimia takriban ‘40‘ ndani ya saa
mbili. Ni hatua kubwa sana
kwa wanaojua takwimu.
Watu
wote waliowahi kuembelea blogu yangu tangu ianzishwe wamefikia ‘2380‘ mpaka
hivi ninavyoandika. Hivyo usingoje kusimuliwa mafanikio haya yanasababishwa na nini,
nadhani wadau wangu wanapenda vitu mchanganyiko.
Huwa
ninajaribu kuandika kila ninachokiona na kupiga picha kila kinachojipitisha
katika kamera yangu, sitaki mchezo.
Napokea
marekebisho na ushauri wa aina yoyote juu ya kuifanya blogu hii kuwa imara na ya
kihabari zaidi, kila unapohisi kuna habari unataka itolewe usisite kuwasiliana
na mimi kwa namba za hapo chini na barua pepe.
Nawashukuru
sana kuwa pamoja nami kupambana na umaskini,
kipo kitu nitaongea kesho juu ya ahadi niliyompa rafiki yangu Evans Musoka, vipi
nitapambana na umaskini nilipokuwa mgeni wake nchini Kenya .
HAFIDH
KIDO
DAR
ES SALAAM , TANZANIA
0713
593894/ 0752 593894
hafidhkido@yahoo.com

No comments:
Post a Comment