Makachero wa Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wamemsafirisha kutoka Dar es Salaam kumleta ZanzibarMeneja wa Meli
ya Skagit Bw Omari Hassan Mnkonje(50) ili kuunganishwa na watuhumiwa wengine
wanaohojiwa na Polisivisiwani hapa.
Naibu Mkurugenzi wa
Upelelezi Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amesema kuwa meneja huyo wa ambaye ofisi
zake zipo Jijini Dar es Salaam ameunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi
hiyo.Meneja huyo alikuwa akishikiliwa na Polisi Jijini Dar es Salaam mara baada
ya kutokea kwa ajali hiyo na kwamba ataunganishwa pamoja na wenzake wengine
waliokuwa wakihojiwa na Polisi Visiwani hapa.
Katika hatua nyingine
Kamanda Ilembo amesema kuwa watuhumiwa watatu kati ya sita waliokuwa wakihojiwa
kuhusiana na tukio hili wamewaachiliwa baada ya kuonekana kuwa hawahusiki
katika tukio hilo .
Waliohojiwa na
kuachiliwa huru ni pamoja na Fundi wa zamu wa meli hiyo Bw. Hamis Mbarouk
Juma(60) ambaye naye alikuwa miongoni mwa manusura katika ajali hiyo.Wengine
walioachiliwa baada ya mahojiano hayo ni Mtaalamu wa Vifaa katika meli hiyo Bw.
Ahmed Mashaka
Mbarouk(51) mkazi wa Vikokotoni na Mhudumu wa Meli hiyo Bw. Shaibu Godfrey
Francis Kanuti(33), mkazi wa Tombondo mjini Zanzibar.Watuhumiwa wanaoendelea
kushikiliwa na Polisi liobaki katika kesi hiyo na ambao watafikishwa mahakamani
siku za usoni Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara watakapokamilisha
masuala ya mahojiano.Wakati huo huo, Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
wanaoshiriki katika kazi ya utafutaji wa maiti leo wamefanikiwa kuzipata maiti
nyingine watano na kufanya idadi ya maiti zilizopatikana hadi sasa kufikia 78.
Miongoni mwa maiti
zilizoopolewa leo, moja imetambuliwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania JWTZ Kikosi cha Bendi Zanzibar STG Suleiman Pandu Jape.
Katika Maiti
zilizopatikana leo, nne zilikuwa za wanaume akiwemo mtoto mdogo na mmoja ni ya
mwanamke ambapo kufuatia kuharibika kwa miili hiyo, Kamishna wa Polisi zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuwa maiti
hizozimefanyiwa mazishi katika makaburi ya pamoja yaliyopo eneo la Kama nje
kidogo ya mji wa Zanzibar .
No comments:
Post a Comment