Anthony Kayanda, Kigoma
na Fred Azzah Dar
IKIWA imebaki miaka
mitatu kabla ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini mwaka 2015, wabunge wawili
vijana wamewataka wakazi wa Mkoa wa Kigoma kujiandaa kumpata kutoka eneo hilo .
Kauli za Wabunge hao
zimekuja kipindi ambacho mchakato wa Katiba unaendelea huku kukiwa na uwezekano
wa umri wakugombea urais kushuka hivyo kuwawezesha wanasiasa wengi vijana
akiwamo Zitto, kugombea nafasi hiyo.
Wakizungumza katika
tamasha kubwa lililokutanisha mamia ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma, Deo
Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM), Joshua Nasari wa Arumeru
Mashariki (Chadema) na Halima Mdee, Kawe (Chadema), walisema wanaamini Rais wa
2015 atakuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini na ambaye ni mzaliwa wa mkoa huo.
Katika kauli yao hiyo, wabunge hao
walisema Mbunge huyo ameonyesha umahiri mkubwa katika kusimamia mambo ya
kitaifa bila upendeleo, jambo linalomfanya kujijengea umaarufu mkubwa ndani na
nje ya nchi, hivyo kuonekana wazi kulibeba vema kundi la Vijana wa Taifa hili.
Akimzungumzia kuhusu
rais ajaye kutoka Kigoma, Filikunjombe alisema kundi la vijana lazima liungane
kuhakikisha kuwa linatoa viongozi watakaopigania maslahi yao na Taifa kwa jumla ili kuleta ukombozi wa
kifikra na kimaendeleo kwa maslahi ya jamii.
"Lazima mtambue
kuwa, Tanzania
ni nchi yetu sisi wote na lazima vijana wote bila kujali itikadi zetu za
kisiasa tunatakiwa kujipa moyo kwamba tunaweza kufanya makubwa katika kuleta
maendeleo ya jamii katika nchi yetu," alisema Filikunjombe na kuongeza:
"Vijana wa Kigoma
mnabahati ya kuwa na Wabunge wazuri na ninaamini miaka michache ijayo lazima
mkoa huu utoe Rais wa Tanzania ."
Huku akishangiliwa na
umati mkubwa wa watu waliokusanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini hapa
kuhudhuria tamasha hilo
lililopambwa na wasanii nyota wa kizazi kipya kutoka Mkoa wa Kigoma,
Filikunjombe alisema; "Zitto anastahili kuwa rais".
Mbunge huyo wa CCM
ambaye katika siku za karibuni ameonekana kuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa
Zitto na Chadema, alisema Zitto anafaa kuwa Rais kwani amefanikiwa
kuwaunganisha watu na kuleta umoja miongoni mwao, jambo ambalo linadumisha
umoja wa kitaifa.
Chanzo
No comments:
Post a Comment