Watafiti hao wanasema kuwa wamepata njia ya
kuviondoa virusi vinavyo sababisha ukimwi mwilini kutumia dawa ya kukinga
saratani.
Virusi
vya ukimwi mara nyingi huwa huishi mwilini kwa miaka mingi bila ya kutambulika,
hivyo kuifanya kuwa vigumu kutibu ugonjwa huo.
Katika
nyaraka zao kwenye jarida la matibabu la Nature, watafiti hao wanasema kuwa
wamepata njia ya kuvimulika virusi hivyo mwilini na kuwa baada ya kufanya hivyo
wameweza kuviua kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.
Tayari
majaribio kwa wagonjwa wanane zimefanikiwa.
Hata
hivyo wamesema kuwa bado kunahitajika utafiti zaidi wa kuwezesha kuundwa dawa
marudufu ya kumaliza ugonjwa huo.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment