Mashirika ya kupigania
haki za kibinadamu yameishutumu serikali ya Kenya kwa kukataa kugharamia kesi
ambayo wapiganaji wa zamani wa Mau Mau wameishitaki serikali ya Uingereza.
Wapiganaji
hao wazamani tayari wamewasili Mjini London kushitaki wakoloni walioitawala Kenya kwa madai ya kuwatesa wakati wakipigania
uhuru wa Kenya .
Awali serikali ilitangaza kuwa inaunga mkono
kesi hiyo ya Mau Mau. Lakini wakuu wa serikali wameshindwa kueleza ni kwa
sababu gani hawagharimii kesi hiyo.
George Morara alihoji kwanini serikali ya Kenya haitaki kuwasaidi Mau Mau ambao
walipigania uhuru wa Kenya
wakati serikali hiyo hiyo sasa inawasaidia wakenya mashuhuri ambao
wameshitakiwa katika mahakama ya uhalifu wa kimataifa-ICC.
Mwanaharakati
huyo amesema kuwa ingawa Mau Mau ilikuwa maarufu katika miaka ya 1950 hadi 60
lakini kuna baadhi ya viongozi wa serikali wanaohofia kuwa kesi hiyo huenda
ikawadhuru kisiasa.
Mwandishi
wa BBC wa Maswala ya Afrika Martin Plaut anasema imechukua muda mrefu kwa kesi
hiyo kufikia hatua ya sasa na huenda ikachukuwa muda mwengine mrefu zaidi kwa
Mau Mau kuthibitisha madai ya kuteswa na wakoloni wakati wakipigania uhuru wa Kenya .
Chanzo:
BBC swahili

No comments:
Post a Comment