Baraza La Habari
La Kiislamu Kuwafungulia Kesi Mahakamani Madaktari Waliogoma
Baraza la Habari la
Kiislamu Tanzania (BAHAKITA) limesema linakusudia kuwafungulia mashitaka
Madaktari Mabingwa wote pamoja na Madaktari waliokuwepo kwenye Mafunzo kwa
Vitendo (Interns) ambao walishiriki katika mgomo kwenye hospitali mbalimbali
nchini na kusababisha wagonjwa kukosa huduma za matibabu huku wengine
wakipoteza maisha yao .
Hatua hiyo imefikiwa
baada ya baraza hilo
kukaa na Madaktari waliokua katika mgomo na kukubaliana kuwa waiombe radhi
Serikali pamoja na wananchi kisha warudi kazini, lakini Madaktari hao wamekiuka
makubaliano hayo na kuendelea na mgomo jambo lililoonyesha kwamba hawakuwa
tayari kupata suluhu.
Katibu wa BAHAKITA, Said
Mwaipopo amesema wameshauriana na Wanasheria wao na kuamua kuwafungulia kesi ya
mauaji Madaktari hao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam tarehe 16 Julai 2012.
Amesema, “kwa tukio zima
jinsi lilivyokwenda, limeonyesha kwamba Madaktari hawataki wala hawana shida
tena ya kurudi kazini kwa sababu ni wazi kwamba kuna mtu yuko nyuma yao wanaemtumikia. Sisi
kama Watanzania, sehemu ya jamii tumekaa na Wataalamu wetu wa Sheria
tumekubaliana kwamba Jumatatu tunakwenda kufungua kesi Mahakamani kwa Madaktari
wote waliogoma wakati wamesomeshwa na kodi zetu na Serikali yetu imewasomesha,
tutawafungulia kesi ya kusababisha mauaji pale Muhimbili, kwa hiyo tunachofanya
hivi sasa ni kwenda pale Muhimbili kwa mganga mkuu kuchukua orodha ya watu
waliopoteza maisha.”
“Sisi tuliingilia kati
mgomo huu kwa nia njema ya kutapata suluhu kati ya madaktari na serikali…lakini
baada ya taarifa zetu kutoka kwenye vyombo vya habari Ikulu ilitoa tamko la
kukataa kukutana na sisi... ...lakini Ikulu walieleza vizuri kwamba hawajawahi
kukataa kukutana na viongozi wa madaktari kwa maana hiyo basi serikali
imeonekana dhahiri kutaka suluhu. Baada ya taarifa hizo sisi tuliwatafuta
viongozi wa MAT ambao tuliwaeleza kwamba kutokana na taarifa hizo wao waombe
msamaha kwa serikali na umma wa watanzania kwa kuendesha mgomo ambao
umesababisha vifo. Lakini baada ya kuwaeleza hivyo hawa viongozi wa MAT
hawakukubali…sisi kama viongozi ambao lengo
letu ilikuwa kutafuta suluhu tukaona hawa vijana (madaktari) wana nia mbaya.
Lakini sisi si kujitoa tu bali tutawafungulia mashtaka ya mauaji wote
walioshiriki katika mgomo huo. Tutafanya hivyo ili fundisho kwa wengine ambao
wana nia kama za madaktari wanaoendesha
migomo.
Kwa hiyo sisi tunaunga
mkono kufikishwa mahakamani kwa Rais wao ni njia sahihi kabisa ya kurudisha
nidhamu, lakini pia tunaunga mkono matamko yote yaliyotolewa na serikali dhidi
ya madaktari,”alisema Mwaipopo.
Akijibu hoja hizo,
Katibu wa MAT, Dkt. Edwin Chitage amesema hawaogopi kufikishwa mahakamani na
kwamba wao waliwapokea viongozi hao kwa nia njema wakiamini ni viongozi wa
dini.
“Kama
wamesema watatufikishwa mahakamani wao waende halafu tutakutana nao…sisi
tuliwapokea kwa nia njema kabisa kwa sababu walituomba wenyewe..lakini baada ya
kikao cha Jumamosi siku ya Jumapili wakatupigia simu kuomba tukutane nao,sisi
tulikutana nao lakini cha kushangaza walitueleza kwamba wamepigiwa simu na mtu
wa Ikulu akiwataka kutuambia kwamba inabidi tuandike barua ya kuomba msamaha
halafu tuwape wao ili waipeleke…sisi tulishangaa jambo hili… sisi hatutafanyi
kazi hiyo,” alisema Dkt.Chitage.
Chanzo: http://www.wavuti.com
</
No comments:
Post a Comment