Rais
Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mdogo wa
Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Bw. Stephen O'Brien jijini London , ambapo Uingereza iliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika
mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuendeleza sekta ya
nishati hususan utafutaji wa gesi asilia.
Kikwete amehutubia mkutano wa kwanza wa aina yake duniani
ulioanzisha Mchakato wa Dunia wa kuwawezesha wanawake katikanchi maskini kuweza
kupata taarifa sahihi juu ya kupanga uzazi bora.
Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Queen Elizabeth II
jijini London July 11, 2012 utalenga kuwawezesha
wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari,
huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Mbali na mkutano huo Rais Kikwete alifanya mazungumzo na
kampuni ya gesi asilia ya British Gas (BG Group) kampuni hiyo imewekeza kiasi cha Pauni 80 za
Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini
Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi
katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara.
Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group
mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai
11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo
yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla
ya wafanyakazi 6,000.
NB: Habari hii imehaririwa na Kido Jembe lakini habari kamili
imetolewa kwa hisani ya mjengwa blog.



No comments:
Post a Comment