Wednesday, July 11, 2012

Mtaani kwetu..

 Mtaani kwetu watoto huwahi kuamka hata sijui ni kwanini labda hawana magodoro..

Kila kukicha lazima ukateke maji bombani sio kisimani.. kwanini wasiyavute nao wawe na mabomba yao? Swali gumu eennhh.....

 Miguu ya kuku ni mitamu jamani hebu jaribuni nanyi siku moja. Mtaani kwetu ni kitoweo cha kawaida tu.

 Mtaani kwetu wanamama wakiamka hawavai magauni mpaka ikifika mchana baada ya kupika, ni mwendo wa khanga tu, mchana kutwa
.
 Mtaani kwetu maduka ya urembo 'cosmetics' yanatembea 'mobile' haina haja ya kupata tabu.

Nikikwambia mtaani kwetu watoto wanawahi kuamka namaanisha,usifikiri huu ni mchana asubuhi hii,ati wanapika chai...

No comments:

Post a Comment