Ndugu zangu,
Matarajio yangu yamekuwa sahihi na Dk Shein amevuka kizingiti cha kuvuruga utaratibu wa Serikali za umoja wa kitaifa kwa kuamua kumteua ndugu Rashid Suleiman Seif, kutoka jimbo la Ziwani Pemba kushika nafasi ya uwaziri wa mawasiliano Zanzibar.
Rashid anatoka chama cha wananchi CUF, hivyo kuwafanya jamaa kutokosa nafasi hiyo kwa ndugu yao kujiuzulu zaidi hali hiyo imezidi kuwaongezea umaarufu CUF kwa kuonekana ni chama makini ambacho kinajali wananchi.
Pia zipo taarifa leo Dk Shein ametangaza tume ambayo itachunguza kuzama kwa meli hiyo, ambapo kwa taarifa za awali nilizopata ni kuwa tume hiyo pia ndiyo iliyochunguza ajali ya awali ya MV Spice Islander...
Nitaendelea kuwapa taarifa kadiri ninavyozipata.....
No comments:
Post a Comment