Hapa nikiwa na jembe langu Danny, pembeni ni mama yake marehem Charity nyumbani kwao Kiluvya leo.
Hapa nikiwa na dada wa majembe Editha, rafiki karibu wa marehem jembe la mass comm hili KIU. Maskini amemaliza chuo akiwa mpweke 'classmate' wake Mungu amempenda zaidi. Akijifariji na mama Tunda.
Hawa ni mama wa marafiki wawili vipenzi. Kushoto ni mama yake Editha na kulia ni mama yake Charity.
Na Hafidh Kido
Mwaka mmoja sasa umefika
tangu uondoke dada yetu Charity Tunda, najua inatosha sasa kuhuzunika ila moyo
wangu ulifanya simanzi niliposimama mbele ya kaburi lako na akili ikanambia
ndani ya nyumba ile ya milele kumelala mifupa baridi ya mtu niliemthamini na
kumpenda sana .
Hata sasa siwezi kusahau
tabasamu lako na kicheko cha kutia matumaini, pia siwezi kusahau huruma yako
kila nilipokuja katika chumba chako tukiwa chuoni Kampala , vinywaji vya maji ya matunda,
chakula na kutazama Ze Comedy kwenye kin’gamuzi chako. Pia sitosahau namna
ulivyokuwa ukinilazimisha kuja kukutembelea kila nilipokutupa. Bado natamani
kusafiri basi moja ukiwa pembeni ya kiti tukielekea chuoni.
Yataonekana ni mambo ya
kijinga kuyakumbuka lakini kwangu yalikuwa na maana sana kwa umri tuliokuwa pamoja. Sitosahau namna
ulivyokuwa ukiipenda picha ya mwanangu Hafidh jr, kila nilipoingia chumbani
kwako nilifarijika namna ulivyokuwa ukiitandaza kwenye meza picha ile.
Hatuna cha kufanya zaidi ya
kumuomba Mungu akupokee vema na akusamehe kila baya ulilofanya ukiwa duniani.
HAFIDH KIDO
0713 593894/ 0752 593894
DAR ES SALAAM , TANZANIA
www.Kidojembe.blogspot.com




No comments:
Post a Comment