Wednesday, December 26, 2012

Acheni midomodomo Shaaban Kado ni mali ya Coastal Union kwa sasa....

Mwenyekiti wa Coastal Union ya Tanga Hemed Hilal 'Aurora' kushoto na Makamu Mwenyekiti Steven Mnguto kulia wakiwa wamekamilisha kazi ya kumsainisha Mlinda mlango mpya wa timu hiyo Shaaban Kado.

Kwa wiki kadhaa kulikuwa na mvutano baina ya vilabu vitatu hivi Yanga, Mtibwa na Coastal juu ya usajili wa Kado kwani Mtibwa walipewa Kado kwa mkopo kutoka Yanga lakini wanalalamika kuna kiasi cha fedha hakijaingia kwao kwa kuuzwa Kado.

Lakini leo mwenyekiti wa Coastal alizungumza katika kipindi cha Sports Extra kinachorushwa na Clouds FM kwa njia ya simu na kuweka wazi kuwa wameshamalizana na Yanga na sasa Kado ni mchezaji halali wa coastal....

No comments:

Post a Comment