Saturday, December 8, 2012

Haya twendeni kwenye kongamano la uhuru kesho....

UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM Academic Staff Assembly 

TAARIFA KWA UMMA 

Hii ni kuitaarifu jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na umma kwa ujumla kuwa, katika kusheherekea uhuru wa Tanzania Bara, Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) kwa ushirikiano na IPP Media wameandaa Kongamano la Uhuru litakalofanyika siku ya Jumapili tarehe 9 Desemba 2012 katika Ukumbi wa Nkrumah kuanzia saa 8 alasiri hadi saa 12 jioni. 

Mada kuu ya Kongamano ni, “Uhuru wetu na Mustakabali wa Taifa kwa Miaka 50 Ijayo”. Kongamano hilo litajikita katika vipengele vifuatavyo:- 

a) Amani na Utulivu wa Taifa letu kwa Miaka 50 Ijayo; 

b) Elimu na Maendeleo ya Taifa kwa Miaka 50 Ijayo; 

c) Rasilimali zetu kwa Maendeleo ya Kiuchumi ya Taifa.

 Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV, Radio One na Capital Radio ili wananchi wote waweze kufuatilia kongamano hilo muhimu. Watakaongoza mjadala ni Prof. Gaudence Mpangala, Dkt Martha Qorro, Dkt Haji Semboja, Dkt. Kitila Mkumbo, Bw. Maggid Mjengwa na Mhandisi Joshwa Raya. Watakuwepo pia wazungumzaji waalikwa kama vile: Mzee Joseph Butiku, Dkt Aldin Mutembei, Mh. January Makamba (Mb), Julius Mtatiro, Usu Mallya na Esther Wassira. Kongamano linategemewa kufungwa na Mh. Bernard Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

 Wote mnakaribishwa..

Limetolewa na Uongozi wa UDASA

No comments:

Post a Comment