Kufuatia ya moja kati ya mauaji makubwa kutokea katika
historia ya Marekani, wanasiasa akiwemo Rais Barack Obama, wametaka sheria
kuhusu umiliki wa bunduki nchini Marekani zibadilishwe, ili kuepusha maafa kama hayo siku za usoni.
Akizungumza baada ya mauaji ya watoto na watu
wazima 26 katika shule moja ya msingi katika jimbo la Connecticut Ijumaa, Rais
Obama aliyeonekana kujawa na huzuni, alitoa wito kuchukuliwe hatua ya maana
kuzuwia mauaji kwa kutumia bunduki.
Hakutoa
maelezo zaidi.
Taarifa
zaidi zimejitokeza kuhusu yaliyotokea katika mauaji hayo katika shule ya msingi
ya Sandy Hook mjini Newtown .
Mshukiwa
mwenye umri wa miaka 20 - aliyeitwa Adam Lanza - alimuuwa mama yake nyumbani
kwake, kabla ya kuelekea katika shule hiyo na kuwafyatulia risasi wanafunzi.
Walioshuhudia
walisema walisikia zaidi ya milio mia moja ya risasi na kuwaona watoto waliokuwa
wakihofia maisha yao
wakilikimbia jengo.
Wanafunzi
hao walikuwa kati ya umri wa miaka mitano na kumi.
Wakaazi
wa Newton
wamekesha wakiomboleza.
Rais
Obama ametoa amri kuwa bendera zipepee nusu mlingoti kwenye majengo ya taifa.
Akizungumza
juu ya mauaji hayo, waziri mkuu wa Australia ,
Julia Gillard, alisema tukio hilo
limezidi kusikitisha kwa vile waliouwawa ni watoto.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment