Rais Jacob Zuma amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa
kiongozi wa chama tawala nchini humo cha African National Congress ANC.
Zuma
alipata idadi kubwa ya kura zilizopigwa na wajumbe elfu nne wa chama hicho
wakati wa mkutano wao uliofanyika Mangaung.
Tangu
mwanza wa zoezi hilo ,
Rais Zuma, alitarajiwa kushinda na idadi kubwa ya kura dhidi ya mpinzani wake
wa pekee ambaye pia ni naibu makamu wa rais Kgalema Motlanthe.
Bwana
Motlanthe sasa amepoteza nafasi yake ya naibu kiongozi wa chama hicho na mahala
pake pamechukuliwa na mfanyabiashara maarufu na mwanaharakati dhidi ya ubaguzi
wa rangi Cyril Ramaphosa, ambaye sasa atakuwa makamu wa rais wa Afrika Kusini.
Ramaphosa
makamu mpya wa rais
Mshindi wa nafasi hiyo ndiye atakayekuwa na
nafasi ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2014.
Chama
cha ANC kimeshika hatamu nchini Africa Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa
ubaguzi wa rangi mwaka 1994.
Polisi
nchini humo, hapo jana waliwatia mbaroni watu wanne baada ya taarifa kuzagaa
kwamba walikuwa na mpango wa kulipuwa ukumbi unaotumiwa na wajumbe hao wa chama
cha ANC.
Baada ya uchaguzi huo kucheleweshwa kwa masaa kadhaa, zoezi
la kupiga kura lilianza saa sita usiku na kukamilika majira ya saa moja asubuhi
kwa saa za Afrika Kusini.
Wajumbe hao walioonekana wamechoka huku
wakijifunika mablanketi walionyesha vidole vyao vikiwa na alama ya wino.
Wajumbe
hao wamekuwa wakipiga kura kwa ajili ya nafasi ya uongozi wa juu wa chama
hicho.
Wafuasi
wa rais Zuma, tayari wanaendelea kusheherekea, kufuatia ushindi huo mkubwa.
Rais
Zuma analaumiwa kwa kushindwa kupunguza umaskini au kutatua tatizo la ufisadi
ndani ya chama cha ANC na serikali, wakati mwezi wa nane mwaka huu watu walishangazwa
na jinsi polisi walivyowapiga risasi na kuwauwa wachimba madini 34 ambao
walikuwa wamegoma.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment