Friday, December 14, 2012

Coastal mpaka vijana wake wanatisha jamani...

Leo jembe nilikuwa na ndugu zangu kuenda kutazama shndano la Uhai Cup linaloshirikisha timu B ambazo zina vijana wa chini ya miaka 20 kutoka timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

Timu ya Coastal Union inafanya vizuri sana katika michuano hii, tangu walipoanza tarehe 11 mwezi huu wamecheza mechi tatu ya kwanzA ilikuwa dhidi ya Prison ya Mbeya ambapo vijana wa Coastal walishinda 2-1. wafungaji wakiwa ni Yussuph Chuma na Ramadhan Shame 'Batista',

Mechi ya pili ilikuwa ni dhidi ya Toto Africa ambapo Coastal walishinda 3-1, wafungaji wakiwa ni Muddy Miraji, Mohammed na Abdi Banda. katia mchezo wa leo uliocheZwa uwanja wa kumbukumbu ya Karume saa nane mchana Coastal walikipiga na JKT Ruvu ambapo bado vijana wa coastal walitoka kifua mbele kwa kushinda goli moja lililofungwa na Hamad Juma.

Bado wamebakisha mchezo mmoja dhidi ya Mtibwa sugar itakayochezwa uwanja wa Karume siku ya jumatatu saa nane mchana. Hata hivyo kwa mujibu wa msimamo Coastal tayari imeshajihakikishia kuingia hatua ya robo fainali kwani wanaongoza katika kundi lao kwa point tisa. Maana yake katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa hata wakipoteza ama kutoka suluhu bado wanayo nafasi kuendelea na michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Bakhresa chini ya kinywaji chake cha maji safi ya Uhai.

Mungu ibariki timu yetu ya vijana ambayo imeonekana kusukwa vyema kiasi timu nyingine za vijana zinaogopa kila wanaposikia wanapangwa na timu hiyo.

Coastal chini ya miaka 20 mwanzoni mwa mwaka huu ilishiriki kwa mara ya pili kombe la Rolling Stone lililoshirikisha vijana wa timu zinazotoka afrika mashariki na kati, ambapo Coastal mBali ya ugeni wao walifanikiwa kuingia fainali ambapo walifungwa kwa matuta na timu ya Congo na hivyo kuishia kushika nafasi ya pili na kuacha gumzo katika jiji la Bujumbura nchini Burundi ilipofanyika michuano hiyo.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
14/12/2012

No comments:

Post a Comment