Monday, December 24, 2012

Ziara ya makamu wa Rais Unguja eneo la Mkokotoni Shangani.

 Hii picha nimeipenda sana... viongozi wetu wanaona matatizo na mazingira magumu wanayoishi wananchi wao, lakini wanaishia kuwapa mikono na kupiga nao picha hakuna hatua yoyote inayofanyika kuondoa hali hizo...

 Makamu wa Rais akiwa na mzee Haji Machanu Ngwali ambae anasumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba miguu kutokana na uzee, Dk Bilal alikuwa katika ziara yake mjini Unguja Mkokotoni Shangani mkoa wa Kaskazini
Bilal akiwa na mkewe mama Asha Bilal wakati walipomtembelea mzee Haji Machame ambae pia anasumbuliwa na miguu.

 Mzee Juma Muhidin Mohammed aliekaaa kulia akiomba dua pamoja na makamu Rais Mohammed Bilal katika ziara hiyo Unguja... Mzee huyu pia anasumbuliwa na miguu kutokana na usee..

                        Makamu wa Rais Bilal akiwa na mzee Ali Mohammed Juma katika ziara hiyo.

Kidojembe imegundua kitu kimoja, wazee wengi wa pwani wanasumbuliwa na maradhi ya kuvimba miguu, kama blog hii itawezeshwa kufika vijiji vya pwani itaweza kurudi na matokeo mazuri ya utafiti kuhusu tatizo hili. Naam blog za kijamii lazima ziangalie masuala ya kijamii kwa kina, tatizo lipo na linataka utatuzi....

Picha zote kwa hisani ya ofisi ya makamu wa Rais.

No comments:

Post a Comment