Thursday, December 20, 2012

Tunaendelea... hatimae penalt zikatimia Coastal 4 Ruvu Shooting 3.... Nusu fainali hiyoooo

                             Viongozi wakashindwa kujizuia... Golikipa ndie kamanda siku hiyo...

                                             Baada ya penalt ya mwisho ikawa furaha tupu.

 Unapakumbuka hapa? Katika zile picha za awali eneo hilihili niliwapiga hawa maswahiba wakiwa wamenunaaa wanajua safari ya Tanga inawahusu. Hapa wanacheeekaaa. Maalim Ubinde anamwambia shemeji yake, si nilikwambia mjombaaaaa acha hofu... kumbe hata yeye alikuwa na hofu.. ahahaaaa

                                                                  Kukumbatiana kukafuata..

 Lakini mfungaji wetu wa mabao mawili Mohammed Miraji (Muddy magoli) akawa ameumia vibaya kifundo cha mguu, hii ni baada ya mechi kuisha wenzake wanafurahia ushindi yeye anaugulia maumivu. Sijui kama atakuwepo katika kikosi cha leo dhidi ya Simba U/20.

Baadae Muddy magoli nilimuona akiwa na furaha nikaamua kupiga picha hii nikamwambia wewe ndie man of the match, akacheeeeka.

No comments:

Post a Comment