Na Mahmoud Zubeiry, Kinshasa
AZAM FC ya Dar es
Salaam, imefungwa mabao 2-0 na Shark FC ya hapa, katika mchezo wake wa mwisho
wa Kundi B, Kombe la Hisani, kwenye Uwanja wa Martyrs jana jioni.
Mabao ya washindi,
timu inayomilikiwa na mdogo wake rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
Joseph Kabila yalifungwa na Ndibu Kalala dakika ya 23 na Kalala Kabongo dakika
ya 34.
Hata hivyo, kipigo
hicho kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na uchezeshaji mbovu wa marefa, ambao
tangu mwanzo walionekana kuwapendelea wenyeji.
Azam leo imenyimwa
penalti mbili za halali, moja kila kipindi, ya kwanza baada ya shuti la
mshambuliaji Gaudence Mwaikimba kuzuiwa kwa mkono na beki wa Shark na ya pili
kiungo Humphrey Mieno aliangushwa kwenye eneo la hatari, tena ndani ya sita
akiwa amekwishamtoka kipa, lakini zote refa akapeta.
Washika vibendera nao
walizima mashambulizi kadhaa ya Azam kwa kudai wachezaji walikuwa wameotea.
Mabao yote Azam
walifungwa wakitoka kushambulia na hayakuwa na mushkeli, makosa ambayo
walirekebisha na hawakuyarudia kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza, timu
zilishambuliana kwa zamu, lakini kipindi cha pili Azam walitawala zaidi mchezo
na kama si ‘madudu’ ya refa, matokeo yangeweza
kubadilika.
Kwa matokeo haya,
Shark inaongoza Kundi B kwa pointi zake tatu, ikifuatiwa na Dragons iliyotoka 1-1
na Azam katika mchezo wa kwanza.
Azam sasa itaomba
Shark iifunge zaidi ya mabao 2-0 Dragons katika mechi ya mwisho ya kundi hilo Desemba 23, ili
ifuzu kuingia Nusu Fainali.
Azam imecheza mechi
zote mbili bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi
wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani
Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivory Coast,
kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Nusu Fainali
zitachezwa Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka
mshindi wa tatu. Kundi B, lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC
MK na Real De Kinshasa.
Kocha wa makipa, Iddi
Abubakar aliyeiongoza timu hiyo katika mechi hizo mbili alilalamikia
uchezeshaji wa marefa, ambao walisindikizwa na Polisi kutoka uwanjani baada ya
mechi, kutokana na kuwakera hata mashabiki wa timu za hapa waliotaka kuwafanyia
fujo.
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Malika
Ndeule/Uhuru Suleiman dk 85, Samih Hajji Nuhu, Luckson Kakolaki/Omar Mtaki dk
65, David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo/Himid Mao dk80, Humphrey
Mieno, Seif Abdallah, Gaudence Mwaikimba na Waziri Salum/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk
65.
meneja msaidizi Jemedari Said ndie anaeifundisha timu.......kocha na msaidizi wake bado wamezuiliwa nairobi kwa kukosa viza.
Chanzo: bin zubeiry blog
No comments:
Post a Comment