Monday, December 24, 2012

Kocha bora na Golikipa bora wa mwaka michuano ya Uhai Cup U/20 watoka Coastal Union.

Bakari Shime kocha bora wa mwaka michuano ya Uhai Cup Under 20 alitawazwa jana na viongozi wa TFF na kupewa zawadi ya laki tatu (300,000) hapa akiwa kazini na vijana wake Coastal.

kama kawaida akizungumza kidogo lazima mabadiliko yaonekane.

 Halafu sifa yake kuu si mpenda majivuno, ukimuona kama mpofu vile haya subiri mapumziko halafu vijana warudi.

                          Halafu hapendi kuzungumza sana, anaangalia zaidi kuliko kuzungumza.

 Umeona balaa hili, katika mechi zote ngumu watoto walikuwa wanatangulia kufungwa lakini wakirudi kutoka mapumziko tu, ni wapya.

Hapa ni baada ya kuwachapa Simba katika nusu fainali waliokuwa wakiogopewa na kila mtu. tuliwapiga 2-1, Kocha alinichekesha kweli tulipokuwa mapumziko, aliwambia wachezaji, "hawa Simba hawana lolote weupe kama hizo jezi mlizovaa.." ahahaaaa

Huyu ndie golikipa bora wa michuano ya Uhai Cup, Mansour a. Mansour wa Coastal Union alitawazwa jana na kupewa kitita cha laki tatu (300,000).

No comments:

Post a Comment