Makamu wa Rais wa Afrika Kusini Montlanthe ndie mpinzani mkubwa wa Rais Jacob Zuma katika uchaguzi wa ANC leo.
Njama ya kushambila mkutano wa wajumbe wakuu wa chama
tawala nchini Afrika Kusini, cha African national Congress ANC, imetibuliwa.
Msemaji wa polisi nchini humo amethibitisha
tukio hilo , na
kusema kuwa washukiwa wanne wenye asili ya kizungu wenya itikadi za siasa kali
wamekamatwa.
Rais Jacob Zuma, na maafisa wengine wakuu wa
serikali na wa chama hicho wanaohudhuria mkutano huo unaoendelea Mangaung,
wamepewa ulinzi mkali.
Viongozi wapya wa chama hicho wanatarajiwa
kuchaguliwa na wajumbe hao.
Chama cha ANC, kimekuwa madarakani tangu
kumalizika kwa utawala wa wazungu walio wachache mwaka wa 1994.
Msemaji wa polisi Phuti Setati, ameliambia
shirika la habari la Reuters kuwa washukiwa wanne ambao walikuwa wakipanga
jinsi ya kuuweka bomu katika eneo la mkutano huo, unaofanyika katika chuo kikuu
cha Free State
iliyoko katika eneo la Mangaung.
Zuma kukabiliana na naibu wake
Mwandishi wa BBC Milton Nkosi, ambaye yuko
katika eneo hilo
anasema, hali ya ulinzi imeimarisha nje na ndani ya ukumbi wa mkutano huo.
Ameongeza kusema kuwa maafisa wa polisi
wanayakagua magari yote na watu wanaoingia katika ukumbi huo kwa kutumia vifaa
maalum na pia mbwa wa kunusa.
Rais Jacob Zuma aliufungua mkutano huo siku ya
Jumapili na anawania muhula wa pili kuwa kiongozi wa chama cha ANC.
Hata hivyo Bwana Zuma, anakabiliwa na upinzani
kutoka kwa naibu wake Kgalema Motlanthe.
Mmoja wa wafanyabiashara tajiri zaidi nchini
Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amemuunga mkono rais Zuma kwa kuwania kiti cha
naibu kiongozi wa chama hicho.
Bwana Ramaphosa alikuwa miongoni mwa watu
mashuhuri waliochangia pakubwa wakati wa mpito kutoka kwa utawala wa kizungu
hadi kwa utawa wa Afrika walio wengi.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, katika eneo
hilo la Mangaung, ambako chama hicho kiliundwa karibu karne moja iliyopita,
rais Zum,a alisema kuwa Afrika Kusini iko tayari kwa awamu ya pili, ambayo
atahakikisha kuafikiwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumu yatayaokuwa na
manufaa kwa raia wa nchi hiyo.
Matokeo ya uchaguzi wa viongozi wakuu wa chama
hicho yanatarajiwa baadaye wiki hii.
Kura za uchaguzi wa uongozi wa chama tawala cha Afrika
Kusini African National Congress, ANC, zinaendelea kuhesabiwa.
Wajumbe
elfu nne wa chama hicho wamepiga kura zao usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa
mkutano wa ANC uliopo Mangaung.
Matokeo
ya kura hiyo yanatarajiwa kutoka baadae leo hii.
Kiongozi
wa chama hicho ambaye pia ni rais wa Africa Kusini, Jacob Zuma, anatarajiwa
kupata ushindani mkali katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo kutoka kwa makamo
wake Kgalema Motlanthe.
Matokeo
kutangazwa leo
Mshindi
wa nafasi hiyo ndiye atakayekuwa na nafasi ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2014.
Chama
cha ANC kimeshika hatamu nchini Africa Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa
ubaguzi wa rangi mwaka 1994.
Polisi nchini humo, hapo jana waliwatia mbaroni watu wanne
baada ya taarifa kuzagaa kwamba walikuwa na mpango wa kulipuwa ukumbi
unaotumiwa na wajumbe hao wa chama cha ANC.
Baada ya uchaguzi huo kucheleweshwa kwa masaa
kadhaa, zoezi la kupiga kura lilianza saa sita usiku na kukamilika majira ya
saa moja asubuhi kwa saa za Afrika Kusini.
Wajumbe
hao walioonekana wamechoka huku wakijifunika mablanketi walionyesha vidole vyao
vikiwa na alama ya wino.
Wajumbe
hao wamekuwa wakipiga kura kwa ajili ya nafasi ya uongozi wa juu wa chama
hicho.
Zuma
kushindana na makamu wake wa rais Bw.Motlanthe
Bw.
Motlanthe alimaliza minong'ono iliyokuwepo kwa kutangaza kuwania nafasi ya Zuma
wiki iliyopita.
Siku
ya Jumatatu, Bw. Motlanthe alisema hatasimama tena kuwania nafasi ya unaibu,
msimamo ambao unaonekana kama njia ya
kujiimarisha.
Kwa
kuzingatia idadi ya kura anazopata kila mmoja, Zuma anatarajiwa kuibuka mshindi
na kwa mujibu wa mwandishi wetu, huu ndio unaweza kuwa mwisho wa Bwana
Motlanthe kisiasa.
Baadhi
ya mashabiki wa rais Zuma, tayari washaanza kusheherekea, wakitarajiwa ushindi
mkubwa.
Mpinzani
mkubwa dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi na mfanyabiashara maarufu Cyril
Ramaphosa naye anagombea nafasi ya naibu kiongozi wa chama, huku wachambuzi wa
mambo wakisema hii inaonyesha jinsi rais Zuma anavyoungwa mkono.
Rais
Zuma analaumiwa kwa kushindwa kupunguza umaskini au kutatua tatizo la ufisadi
ndani ya chama cha ANC na serikali, wakati mwezi wa nane mwaka huu watu walishangazwa
na jinsi polisi walivyowapiga risasi na kuwauwa wachimba madini 34 ambao
walikuwa wamegoma.
Chanzo: BBC Swahili…
Wafuasi wa ANC.....
No comments:
Post a Comment