Ikulu ya rais wa Afrika Kusini inasema kuwa Nelson Mandela
amefanyiwa uperesheni mjini Pretoria, kutolewa mawe ndani ya kibofu nyongo na
anasemekana anaendelea vizuri.
Rais huyo wa zamani
wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 94, alilazwa hospitali juma moja lilopita
kutibiwa mapafu, na ukaguzi ukaonesha mawe hayo kwenye kibofu.
Katika
taarifa iliyotolewa na serikali, imearifiwa kuwa madaktari waliamua
kushughulika na mapafu yake Bwana Mandela kwanza, kabla ya kufanyiwa upersheni
wa Jumamosi.
Wakuu
wa Afrika Kusini wamelaumiwa kuwa hawakuwa wakieleza hali ya Bwana Mandela,
ambayo imechochea wasi-wasi zaidi kuhusu afya yake.
wakati huohuo huko nchini Misri inaripotiwa kuwa.......Wananchi wengi wa Misri
wamejitokeza kushiriki kwenye kura ya maoni kuhusu katiba iliyogawa nchi, huku
kukiwa na ulinzi mkubwa katika duru ya kwanza ya kura hiyo.
Upigaji kura uliongezwa muda wa saa mbili
katika majimbo kumi pamoja na Cairo na Alexandria , ambako kura
inafanywa Jumamosi.
Mkuu
wa jeshi aliiambia BBC kwamba ameridhika na hali ndani na nje ya vituo vya
kupigia kura.
Lakini
upinzani wa ushirikiano wa National Salvation Front umekilaumu chama cha Muslim
Brotherhood kuwa kimefanya udanganyifu kwenye kura.
Upinzani
unasema katiba iliyopendekezwa inaelemea sana
upande wa Uislamu na hailindi haki za raia.
Duru
ya pili ya kura ya maoni itafannywa baada ya juma moja.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment