BIASHARA imeisha. Azam FC imemuuza Mrisho Khalfan Ngassa
kwa dola za Kimarekani 75,000 kwenda El Merreikh ya Sudan ambako amesaini
mkataba wa miaka miwili, utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa dola za Kimarekani
4,000 kwa mwezi huku naye akilipwa dola 50,000 za kusaini.
Awali, Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu
Ngassa wenye thamani ya dola 100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said
Bakhresa akakataa akisema utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu
nyingine.
Sasa Ngassa baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki
na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan
kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida
kucheza hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika.
Azam FC imesema imeweka mbele maslahi ya mchezaji na taifa
kwa ujumla katika maamuzi ya kumuuza Sudan, kutoka Simba alikokuwa akicheza kwa
mkopo. “Hii timu (Merreikh) kila mwaka inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, maana yake huyu mchezaji atakwenda kupata maendeleo na kuja
kuisaidia zaidi Tanzania
katika mashindano ya kimataifa,”alisema kiongozi mmoja wa Azam.
Alipoulizwa kuhusu Simba SC aliyokuwa anaichezea klabu
hiyo, kiongozi huyo alisema wao walimtoa kwa mkopo Ngassa kwenda kwa Wekundu wa
Msimbazi hadi Mei 31, mwakani na mkataba wao ndio unasema hivyo.
“Sisi tuliwapa Simba huyu mchezaji kwa mkopo hadi Mei 31
na wakatupa Sh. Milioni 25, ila tuko tayari kuwarudishia fedha zao walizota,
lakini huyu mchezaji ni mali yetu na hata TFF wanatambua hilo, na
tumekwishamuuza Merreikh,”alisema.
Alipoulizwa kuhusu Simba kusaini mkataba mpya na Ngassa,
alisema; “We uliona wapi dunia nzima timu inapewa mchezaji kwa mkopo halafu
inamsainisha mkataba? Simba lazima ifike wakati waache kurudia makosa, haya
ndio mambo ya Mbuyu Twite sasa,”alisema kiongozi huyo wa Azam.
Katika kukamilisha mauzo ya mchezaji huyo, kiongozi wa
Marreikh akiwa Dar es Salaam mbele ya viongozi wa TFF na Azam, alipigiwa simu
Ngassa aliye hapa Kampala, Uganda na kuhusishwa katika dili hilo, naye
akakubali ndipo mambo yakamalizwa.
Aidha, Azam wameomba TFF ihakikishe kunakuwa na ulinzi
katika kambi ya timu ya taifa mjini hapa, ili Simba wasimfanyie vurugu Ngassa
na kumvuruga kisaIkolojia, wakati ndiyE tegemeo la timu katika kampeni ya
kutwaa Kombe la Challenge mwaka huu mjiini hapa.
Simba wanasema nini
SIMBA SC imesema haitaki ugomvi wala malumbano na Azam FC,
bali wanataka warudishwe fedha zao zote walizotoa kumsaini mshambuliaji Mrisho
Khalfan Ngassa, Sh. Milioni 55 pamoja na faida juu.
Azam FC jana imemuuza Mrisho Khalfan Ngassa kwa dola za
Kimarekani 75,000 (Sh. Milioni 120) kwenda El Merreikh ya Sudan ambako
amesaini mkataba wa miaka miwili, utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa dola za
Kimarekani 4,000 (Sh Milioni 6,) kwa mwezi huku naye akilipwa dola 50,000 (Sh.
Milioni 75) za kusaini.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu jana kutoka Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba
wao walimsajili mchezaji huyo kwa taratibu, ila wanashangaa sasa Azam wanataka
kufanya mambo kinyume cha utaratibu.
“Sisi tuna mkataba na huyu mchezaji, ambao tulisaini na
wao Azam, ambao ilikuwa kama kuununua mkataba wake wa kule Azam, baada ya wao
wenyewe kushindwana na huyo mchezaji. Tuliwapa Sh. Milioni 25 na baadaye
tukaongeza naye mchezaji mkataba wa mwaka mmoja, tukampa Sh. Milioni
30,”alisema Hans Poppe.
Kapteni huyo Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),
alisema kwa kuwa hawataki malumbano na Azam, wanaomba warejeshewe fedha zao na
faida kidogo, kwani mchezaji huyo amenunuliwa akiwa anachezea Simba SC.
Awali, Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu
Ngassa wenye thamani ya dola 100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said
Bakhresa akakataa akisema utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu
nyingine.
Sasa, Ngassa baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki
na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan
kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida
kucheza hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika.
Azam walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka
huu baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya
zamani, Yanga, katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea
benchi na kuiwezesha Azam kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa
na Yanga 2-0, naye kwa mara nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga,
hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa
mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka
mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa
kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18
akipewa gari.
Ngasa nae ana lipi la kusema
MRISHO Khalfan Ngassa amesema kama Simba wanampenda sana,
wapande dau walilotoa El Merreikh ili aghairi kwenda Sudan .
Akizungumza hapa, Ngassa alisema kwamba yeye kama mchezaji
anaangalia maslahi na kwa mshahara mzuri pamoja na dau nono la usajili
alilopewa Matajiri wa Sudan
amelainika na kukubali kujiunga nayo.
Wakati Azam FC imemuuza Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000
kwenda El Merreikh ambako amesaini mkataba wa miaka miwili, kiungo huyo
mshambuliaji amepewa dau la kusaini mkataba wa miaka miwili, dola 50,000 na
atakuwa analipwa mshahara wa dola 4,000 kwa mwezi.
Awali, Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu
Ngassa wenye thamani ya dola 100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said
Bakhresa akakataa akisema utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu
nyingine.
Sasa Ngassa baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki
na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan
kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida
kucheza hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika.
Azam FC imesema imeweka mbele maslahi ya mchezaji na taifa
kwa ujumla katika maamuzi ya kumuuza Sudan, kutoka Simba alikokuwa akicheza kwa
mkopo. “Hii timu (Merreikh) kila mwaka inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, maana yake huyu mchezaji atakwenda kupata maendeleo na kuja
kuisaidia zaidi Tanzania
katika mashindano ya kimataifa,”alisema kiongozi mmoja wa Azam.
Alipoulizwa kuhusu Simba SC aliyokuwa anaichezea klabu
hiyo, kiongozi huyo alisema wao walimtoa kwa mkopo Ngassa kwenda kwa Wekundu wa
Msimbazi hadi Mei 31, mwakani na mkataba wao ndio unasema hivyo.
“Sisi tuliwapa Simba huyu mchezaji kwa mkopo hadi Mei 31
na wakatupa Sh. Milioni 25, ila tuko tayari kuwarudishia fedha zao walizota,
lakini huyu mchezaji ni mali yetu na hata TFF wa natambua hilo, na
tumekwishamuuza Merreikh,”alisema.
Alipoulizwa kuhusu Simba kusaini mkataba mpya na Ngassa,
alisema; “We uliona wapi dunia nzima timu inapewa mchezaji kwa mkopo halafu
inamsainisha mkataba? Simba lazima ifike wakati waache kurudia makosa, haya
ndio mambo ya Mbuyu Twite sasa,”alisema kiongozi huyo wa Azam.
Azam walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka
huu baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya
zamani, Yanga, katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Alifanya hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea
benchi na kuiwezesha Azam kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa
na Yanga 2-0, naye kwa mara nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga,
hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
Ilielezwa kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa
mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka
mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa
kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18
akipewa gari.
Ngassa anang’ara katika Challenge ya mwaka huu mjini hapa,
hadi sasa akiwa amefunga mabao matano sawa na John Bocco wa Azam na wafungana
kileleni.
Chanzo: Bin Zubeir Blog.
No comments:
Post a Comment