Na Aisha Ngoma na Kelvin Matindiko
MWANDISHI wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Shaban Matutu
amejeruhiwa kwa risasi juzi usiku baada ya Polisi wenye silaha kuvamia nyumbani
kwake, Kunduchi Dar es Salaam wakidai kumsaka kibaka aliyekimbilia ndani ya
nyumba hiyo.
Wakati tukio likitokea jana saa 4:00 usiku, kijana aliyekuwa amejeruhiwa kwa bomu na polisi katika vurugu zilizotokea Tegeta wiki iliyopita, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akielezea tukio
Alisema wakati mkewe akielekea mlangoni, alimtaka mtu aliyekuwa akimwita ajitambulishe lakini hakufanya hivyo.
“Wakati mke wangu anajiandaa kwenda kufungua mlango nikasikia sauti za watu wengi wakiongea nje na sauti zilikuwa za wanaume, ikanibidi nimzuie,” alisema Matutu.
Alisema baada ya kumzuia, aliamka na kuchukua panga kwa ajili ya kujihadhari na kwenda kufungua mlango. Lakini kabla ya kuufungua, alishtuka kuona mlango ukisukumwa kwa nguvu hivyo naye kulazimika kuuzuia.
Katika patashika hiyo, anasema alimulikwa kwa tochi yenye mwanga mkali usoni na kisha kusikia kishindo cha bunduki jambo lililomfanya aamini kuwa mkewe ameuawa.
“Sikujua kuwa ni mimi ndiye niliyejeruhiwa nilipomwona mke wangu yupo salama na mimi damu ikiwa inanitoka ndipo nikabaini kuwa aliyejeruhiwa ni mimi,” alisema Matutu.
Alisema baada ya tukio
Aliwakatalia na kuwaomba wampeleke kupata matibabu, wakati huo akiwasiliana na baadhi ya ndugu na jamaa zake kuwapa taarifa ya kilichompata.
Polisi wajitetea
Akizungumzia tukio
Alimtaja askari huyo, F.8991 D/C Idrisa na kueleza kuwa alifika na wenzake katika nyumba hiyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema kuwa kuna majambazi sugu waliojificha humo.
“Askari huyo aliyekuwa na wenzake wanne, baada ya kujeruhiwa alirukiwa na huyo aliyemkata panga, katika purukushani hizo risasi moja ilifyatuka kutoka kwenye silaha aina ya bastola aliyokuwa nayo huyo askari na kumjeruhi kwenye bega la kushoto mtu aliyekuwa akipambana naye,” alidai Kenyela.
Mashuhuda
Baadhi ya mashuhuda akiwamo aliyetoa taarifa za kuwapo kwa uhalifu eneo
Walisema hata baada ya kuelekezwa, askari hao hawakufuata maelezo hayo na badala yake wakaenda katika chumba cha mwandishi huyo pasipokuwa na kiongozi yeyote wa eneo
“Tunachojua sisi katika mazingira kama yale wangekwenda kwa mjumbe lakini hawakufanya hivyo na hata chumba walichokwenda siyo kule tulipowaambia,” alisema mmoja wa watu hao aliyeomba jina
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
“Nilikuwa miongoni mwa watu waliompeleka Matutu Muhimbili na ilipofika saa nane usiku walimhamishia Moi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi,” alisema Kibanda.
Ofisa Uhusiano wa Moi, Jumaa Almas alithibitisha Matutu kufikishwa katika hospitali hiyo na kuongeza kuwa jana asubuhi alipelekwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya kuondoa risasi hiyo.
“Tayari ameshaanza matibabu, saa 2.30 asubuhi alipelekwa katika chumba cha upasuaji,” alisema
Aliyeruhiwa kwa bomu afariki
Majeruhi aliyekuwa amelazwa Muhimbili baada ya kulipukiwa na bomu Novemba 29, mwaka huu katika eneo la Tegeta,
Kifo cha kijana huyo John Paul (16), kimetokana na majeraha hayo ya bomu aliyopata katika vurugu zilizotokea wakati Kampuni ya Udalali ya Mwankinga ilipokuwa ikifanya operesheni ya kukamata magari.
Msemaji Msaidizi wa Muhimbili, Jeza
Waziri alisema jana kwamba kijana huyo alifariki dunia saa sita usiku katika
Wodi ya Sewa Haji alipokuwa amelazwa siku tano zilizopita tangu alipofikishwa
hospitalini hapo.
“Ni kweli amefariki. Tunasikitishwa na kifo chake, madaktari wataeleza baada ya kuandaa ripoti ya kifo,” alisema Waziri.
“Ni kweli amefariki. Tunasikitishwa na kifo chake, madaktari wataeleza baada ya kuandaa ripoti ya kifo,” alisema Waziri.
Marehemu John alikuwa anaishi na dada yake, Davita Tarimo Tabata,
“Siku hiyo aliamka asubuhi nikamwambia aende dukani
Baba mkubwa wa marehemu John aliyefahamika kwa jina la Ephraim John alisema kabla ya mabadiliko hayo walikwenda kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela awasaidie kumsafirisha kwenda nje ya nchi kutokana na hali aliyokuwa nayo.
“
Hata hivyo, alishukuru ushirikiano uliotolewa na Kenyela hasa jitihada zake za kufuatilia kwa karibu matibabu ya marehemu mpaka mauti yalipomfika.
Kwa upande wake, baba wa marehemu, Paul John alisema kutokana na kifo hicho, wamepanga kuwasiliana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ili kuona uwezekano wa kufungua kesi ya madai ya fidia mahakamani.
“Tunasubiri kwanza msiba umalizike ndipo tutakwenda kituo hicho cha sheria kuomba msaada wa kisheria. Hatujui mpaka sasa tufanye nini,” alisema.
Paul alisema walitarajia kuwa na kikao cha wanandugu jana kwa ajili ya kupanga taratibu za mazishi ikiwa ni pamoja na kusafirisha mwili wa marehemu kwenda kijijini kwao Kiraeni, Rombo Mashati, Moshi.
Akizungumzia kifo hicho Kamanda Kenyela alitaka apewe muda ili akusanye taarifa juu ya tukio
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment