Sunday, December 23, 2012

Kunradh wadau wa kidojembe.


                                  Kikosi cha coastal hiki
Ndugu zangu,     
Kwa wapenzi wa timu ya Coastal Union chini ya miaka 20, ambao mlikuwa mkifuatilia michuano ya Uhai Cup yaliyoisha jana kwa timu ya Coastal kufungwa kwa mikwaju ya penalt 3-1 leo sitokuwa na picha za kuwaonyesha.

Najua wengi mlikuwa mkufuatilia picha za matukio kupitia blog hii lakini kidojembe ina ukata wa vifaa vya kazi hasa Camera, hivyo nilikuwa nikiazima Camera ya daktari wa timu, na kwakuwa jana baada ya 'kuvurugwa' kila mtu alishika njia yake maana yake mpaka sasa sijapata picha nilizozipiga jana.

Lakini nawaahidi kesho nitafuatilia picha zile kutoka kwa daktari wa timu na nitawawekea humu ili muone hali halisi ilivyokuwa jana; nachukua fursa hii kuwataka wadau wa kidojembe wenye biashara ndogo na kubwa kutangaza nami ili walau kidojembe iwe na vyanzo vya mapato na kuweza kuondoa matatizo madogo kama haya ya kukosa vifaa vya kazi.

Kumbuka kidojembe ni blog ya kijamii haina mdhamini wala mtu wa kuiwezesha, ni mapenzi tu ya kupasha habari ndiyo yanayoifanya iendelee kuwa hai tangu miezi sita ilipoanzishwa. Kwa sasa blog hii ina wapenzi arobaini elf (40,000) hivyo ni nafasi nzuri kutangaza nasi maana tangazo lako litaonekana na wadau 40,000 kwa wakati wote.

Hata hivyo nimeandaa makala kuhusu michuano ya Uhai Cup na tegemeeni kuiona katika gazeti la Raia Mwema siku yoyote kuanzia leo.

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
kidojembe@gmail.com
+255 752593894/ +255 713593894

No comments:

Post a Comment