Saturday, December 15, 2012

Hatimae mwanazuoni na kadhi wa Zanzibar na Kenya kwa vipindi viwili tofauti Saleh Farsy akumbukwa.....


Sheikh Abdallah Al Farsy enzi za uhai wake. Sheikh Farsy aliwahi kuwa Chief Kadhi wa Zanzibar mwaka 1960, lakini kutokana na sababu za kisiasa alifukuzwa Zanzibar na kuhamia kenya ambapo kutokana na elimu yake kuwa kubwa akafanywa kuwa Chief Kadhi wa Kenya mwaka 1968.

Sheikh Machano Hamad Machano aliekuwa mwanafunzi wa Sheikh Farsy akieleza historia ya maisha ya sheikh huyo na Madrasa pamoja na masomo aliyokuwa akifunza watu wa Zanzibar.. Tamasha hilo lilifanyika katika ukumbi wa peoples Palace Forodhani....

Wanazuoni kutoka Afrika Mashariki wakisikiliza kwa makini habari zinazomuhusu Sheikh huyo aliekuwa na kipawa cha hali ya juu katika masomo ya dini ya Kiislam.

No comments:

Post a Comment