Tuesday, December 18, 2012

Suala la kuanguka jukwaani kwa msanii Sajuki, hakuna haja ya kuwalaumu bongo movie...


Na: Mahmoud Ahmad,Arusha

HALI ya msanii  wa filamu nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha  mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya kuishiwa na nguvu wakati alipopewa kipaza sauti kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama.

Tukio hilo lilitokea juzi jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika  ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid  wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.

Mara baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh” na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.

Hatahivyo,wasanii hao walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika zaidi.

Akihojiwa na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi.

”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
 Hatahivyo,baadhi ya mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali ya msanii huyo huku wengine wakiwatupia lawama nzito baadhi ya wasanii wa filamu nchini walioambatana na msanii huyo kwa madai kwamba wanamtumia ili wapate pesa ilhali mwenzao ni mgonjwa.

Wakihojiwa kwa nyakati tofauti mashabiki hao kwa jazba walisema kwamba msanii huyo alipaswa kupewa muda mwingi wa kupumzika kuliko kuambatana na wenzake mikoani kwani hali hiyo inamchosha zaidi.

“Hawa watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu sana huyu mtu anaumwa sana sisi tunashangaa wanaambatana na mtu mgonjwa mikoani wampe muda apumzike na si kumtumia kwa kupata pesa”alisikika shabiki mmoja akiongea kwa jazba
 Chanzo: Mjegwa blog...

No comments:

Post a Comment