Saturday, December 15, 2012

Tanzania inapogeuka meza ya mazungumzo kwa hatima ya visiwa vya Madagascar....


Rais Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Madagascar Andry Rajoelina mara alipowasili nchini kwa mazungumzo.


Hapa Makamu wa Rais Tanzania dk Gharib Bilal akimuaga Rais Andry Rajoelina baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Kikwete. Wiki iliyopita mpinzani wa Rais wa Madagascar ndugu Ravalomanana ambae aliondolewa madarakani kwa nguvu ya jeshi alikuwa nchini kwa mazungumzo na Rais Kikwete juu ya hatma ya nchi yao.


Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa Tume ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amepewa jukumu na viongozi wenzake ndani ya Jumuiya hiyo kukutana na viongozi wa Madagascar kuwaelezea maamuzi ya mkutano wa viongozi hao wa SADC uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dar Es Salaam.Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii. 
Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao wa SADC wanataka viongozi hao wawili wa Madagascar washawishiwe na wakubali kutogombea katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwakani.

No comments:

Post a Comment