Monday, December 24, 2012

Jana ofisini tulikula keki, ilikuwa siku ya kuzaliwa Mayage S. Mayage alie katika dawati la uhariri....

 Hapa Mayage akizungumza mawili matatu wakati wa kutoa neno la shukurani kwa wafanyakazi wenzie wa kampuni ya Raia Mwema inayochapisha gazeti la kila wiki Raia Mwema.


                                               Ilikuwa ni furaha tuputupu ofisini siku ya jana....

                                     Hapa Mayage akimlisha keki mhariri mkuu Godfrey Dilunga....

                                      Hapa Mayage akimlisha keki meneja masoko John Daniel.

Hakyanani Raia Mwema noma, yaani Mayage anakunywa soda? Mzee wa vitu vikali huyu jamani.


Kwa taarifa tu nina historia kidogo na ndugu Mayage, aliwahi kunifundisha kazi wakati nikiwa kwa mazoezi New Habari mwishoni mwa mwaka 2005, katika gazeti la Mtanzania. Baadae nilipokomaa komaa nikawa naandika makala katika gazeti la Rai nguvu ya hoja, pia akawa ndie anaehariri makala zangu hapohapo New Habari, ila nilipokuwa The African tukawa tunaonana tu ofisini.

Sasa tumekutana tena katika maisha mapya ofisi za Raia Mwema, bado ni mhariri wangu.... Inapendeza sana.... Mungu ampe umri mrefu na afya tele ndugu Mayage mzaliwa wa Kigoma........ Ni mwandishi wa habari nguli kwelikweli..

HAFIDH KIDO
DAR ES SALAAM, TANZANIA
kidojembe@gmail.com

No comments:

Post a Comment