Hapa akiutoka msitu wa mabeki katika moja ya harakati zake kwenye timu ya taifa la Zambia...
Christopher Katongo ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa
BBC mwaka wa 2012.
Naodha huyo wa Zambia mwenye miaka 30 amemshinda
Demba Ba, Didier Drogba, Younes Belhanda na Yahya Toure na kuwa mshindi wa
kwanza kutoka Kusini mwa Afrika katika historia ya mashindano hayo.
Orodha ya washindani hao ilitengazwa na
wataalamu wa soka Afrika, ambao wamezingatia umahiri wa mchezaji, uwezo wa
kiufundi na ushirikiano na wachezaji wengine.
Na idadi kubwa ya watu wamepiga kura kupitia
njia ya mtandao au ujumbe mfupi huku asilimia 40 kati yao wakimchagua Katongo, ambaye anachezea
timu ya China Henan Construction.
Katongo aandikisha rekodi mpya
Huku wachezaji wote walioorodheshwa katika
kinyang'anyiro hicho walikuwa na mwaka mzuri, wanne kati yao walikuwa wameshinda medali mbali mbali,
ni Katongo pekee ambaye mafanikio yake yamezingatiwa na mashabiki wa mpira
Afrika.
Katongo, ambaye ni mwanajeshi nchini mwake,
alikuwa kivutio pindi alipoiongoza Zambia , katika michuano ya kombe la
Mataifa Bingwa barani Afrika mnamo mwezi wa Februari mwaka huu.
Alifunga magoli matatu katika fainali
iliyoandaliwa nchini Equatorial Guinea
na Gabon na baadaye kufunga
bao la ushindi kupitia mkwaju wa penalti na kuisadia Zambia
kunyakuwa kombe hilo .
Katongo afufua matumaini ya Zambia kuelekea
Brazil
Kilikuwa ni kipindi kilichojawa na hisia kwa
Zambia, ambayo miaka 19, iliyopita ilipata msiba mkubwa, pale ndege iliyokuwa
imebeba wachezaji wa timu ya taifa ilipoanguka mita 500 tu mbali na Libreville , na kuuwa
wachezaji wote 25 na rubani wake.
Miezi saba baada ya kuongoza Zambia kushinda kombe hilo ,
Katongo vile vile amekuwa nyota wa timu yake ya taifa wakati wa michuano ya
kufuzu kwa fainali za mwaka ujao,wakati alifunga goli la pekee dhidi ya Uganda .
Bao hilo
liliibuka kuwa bao muhimu sana kwa Zambia
kwa kuwa ilipoteza mechi iliyofuatia kwa bao moja kwa bila, lakini ikafuzu kwa
fainali za mwaka 2013 zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini baada ya kushinda
kwa magoli 9-8 kupitia mikwaju ya penalti.
Mikakati ya kufuzu kwa kombe la Dunia
Na zaidi ya hayo yote, Katongo amechangua
pakubwa harakati za kufufua matumaini ya Zambia ya kufuzu kwa michuano ya
kombe la dunia ya mwaka wa 2014.
Wiki moja baada ya mechi hiyo Zambia ilichuana na Ghana
na Katongo kwa mara nyingine ndiye aliyefunga bao la ushindi na hivyo
kuimarisha matumaini yao
ya kufuzu.
Ikiwa Christopher Katongo ataendelea na hali
aliyo nayo kwa sasa, huenda akaisaidia Zambia
kuandikisha matokeo mazuri wakati wa michuano ya kuwania kombe la dunia nchini
itakayoandaliwa nchini Brazil
miezi kumi na minane ijayo.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment