Thursday, December 13, 2012

FM Academia watimiza miaka 15


Rais wa Bendi ya Muziki wa Dansi nchini FM Academia Nyoshi Elsadaat (Sauti ya Simba, Rais wa Vijana) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 15 ya bendi hiyo tangu kuanzishwa yatakayofanyika jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo, wapili kulia ni Mratibu wa maadhimisho hayo Nasibu Mahinya pamoja na wanamuziki wengine wa bendi hiyo.

Bendi hii awali ilikuwa ikijulikana kama wajelajela Gwaa, ambayo ilitokana na kuvunjika kwa bendi ya wajelajela Stone Musica, ilipata umaarufu baada ya wasanii wake kupelekwa segerea na kutoka na wimbo waliouita Binaadam na kibwagizo chake kikawa ni 'Jelaa jela ni mbaya, jeela jela ni shiida..." ambayo ilikuwa na wanamuziki maarufu kama Nyoshi El Saadat (suti ya simba) mwenyewe, Ndanda kosovo 'kichaa', Maluu Stonche 'Nuhu' Chitoto Pingpong na Pacheko.

kumbukumbu ya kutimiza miaka 15 ya bendi hii iliyojitenga kutoka Wajelajela itafanyika siku ya ijumaa tarehe 14, Dec kesho katika uwanja wao wa nyumbani Msasani Club.

Hafidh Kido
Dar es Salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment