Giraffe Ocean View Hotel
Viongozi wa Double tree wakipewa agiza la kufunga hotel yao jana baada ya kushindwa kufuata taratibu za kulinda mazingira.Waziri Teresia Huvisa kulia akitoa maagiza wakati wa ziara yake leo..
Lulu Mussa na Ali Meja
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais – Mazingira Dk. Terezya Huvisa hii leo ameendelea na ziara ya
kikazi ya kukagua hali ya mazingira katika hoteli zilizopo pembezoni mwa fuke
za bahari ya hindi, jijini Dar es
Salaam .
Ziara ya leo imeanzia katika
hotel ya Giraffe Ocean View, na katika hali ya kushangaza maagizo aliyotoa
Naibu Waziri Charles Kitwanga katika hoteli hiyo mapema mwezi huu ya
kurekebisha mfumo wa majitaka na kuweka fukwe katika hali ya usafi
hayajazingatiwa.
Hatua kali zimechukuliwa dhidi
ya Hotel hiyo ikiwa ni pamoja na kufungiwa mpaka hapo itakapotimiza masharti
yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004.
“Naifunga Hotel hii ya Girafee
mpaka hapo itakapotimiza masharti ya hifadhi ya mazingira” alieleza Dk Huvisa.
Aidha Waziri Huvisa ameipongeza
Hotel ya Beach Comber kwa kuwa na mkakati endelevu wa mfumo wa maji taka na
hifadhi ya fukwe kwa ujumla. Dkt. Huvisa amesema kuwa zoezi hilo ni mkakati
endelevu wa kukagua hoteli zote na viwanda, Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya
Mazingira kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) wanafanya kazi hiyo kwa kikamilifu.
Kwa mujibu wa sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004, Hoteli na Viwanda vyote vilivyoanzishwa kabla ya
matumizi ya sheria hiyo vinatakiwa kufanya (Environmental Audit) na baada ya
sheria ya Mazingira hutakiwa kufanya Tathmini ya Athari za Mazingira (Environmental
Impact Assessment).
Katika ziara ya siku mbili
iliyofanywa na Waziri Huvisa pamoja na Naibu wake Charles Kitwanga imepelekea
kuchukua hatua kali za kisheria ambapo Hotel ya Double Tree na Giraffe Ocean
View zimefungiwa mpaka hapo zitakotimiza masharti waliyopewa.
No comments:
Post a Comment