Ikiwa ni takribani miezi
minne tangu tawi la CHADEMA UK lifunguliwe rasmi na Mr Godbless Lema,
kumekuwepo na maendeleo makubwa ya ujenzi wa tawi hili lakini vile vile
kumekuwepo na changa moto mbali mbali kutokana na uelewa wa watu ktk dhana
nzima ya M4C. M4C ikiwa na maana ya Movement for Change, ni sharti mtu yeyote
anayeingia ktk movement hii kwenye ngazi ya uongozi aelewe haya machache ya
msingi:
1) Kwanza
aone matatizo yanayomgusa yeye na jamii yake
2) Ajue na kutambua fika chimbuko la
matatizo haya
3) Awe tayari kuwa kiini cha mabadiliko
ya kweli anayoyataka kwa jamii
4) Aweze kutoa ufumbuzi kwa kukemea
maovu, kuelimisha na hata yeye binafsi kuelimika
5) Ili
afanikiwe ktk kipengele cha (4) ni sharti ajitambue yeye binafsi ya kwamba ni:
i) Lazima awe safi na mwenye sifa za kukemea waovu
ii) Aweke maslahi ya jamii mbele na si
yake binafsi
iii) Awe na sifa za uongozi zinazotakiwa,
nidhamu ikiwa nambari moja ktk orodha.
iv) Awe na msimamo wa kiitikadi
Kwa hiyo, uongozi wa
CHADEMA UK
kwa baraka za watetezi wa haki ya kweli (CHADEMA TZ) unawatangazia umma
watanzania kokote mlipo kwamba kuanzia leo
tarehe 12/12/12,
Mr Christopher Lukosi amevuliwa rasmi uongozi na amesitishwa uanachama kutokana na kutokidhi mengi ya
yaliyotajwa hapo juu.
Uongozi wa CHADEMA UK unamshukuru sana kwa mchango na ushirikiano wake mkubwa
kwa kipindi ambacho matundu ya chujio yalikuwa makubwa. Tutaendelea kumkumbuka
na hata kutumia misemo yake yenye maana nzito kwa jamii ya kitanzania, kama
vile: -
i) Sisi sote ni ndugu, tatizo ni CCM
ii) Kila kwenye msafara wa mamba na kenge
wamo
Uongozi unamwakikishia
Mr Christopher Lukosi kwamba mamba wote wa CHADEMA UK kwa kushirikiana na wote wenye
kuelewa mageuzi ya kweli
, tutaliondoa tatizo
ifikapo 2015. Tunamtakia kila la kheli katika maisha na ni imani yetu
tutaendelea kuwa ndugu yake baada ya tatizo kutatuliwa !!!!.
“We fail in most of our endeavours because we
too often underestimate People’s Power” [M4C UK , 2012].
Habari hii kwa hisani ya blog ya kaka mjengwa.....
No comments:
Post a Comment