Thursday, December 20, 2012

Jamani eeennhh...!! mechi ya kufuzu nusu fainali iliyopigwa chamazi jana sikuwa na vifaa vya kazi, kidojembe imefulia camera imeharibika napitwa na mengi. Ila niliomba camera ya mdau na leo usiku ndiyo picha nimezipata. zipo nyingi nitakuwa naziweka kwa awamu.... anzeni na hiz kwanza.

 Hapa wachezaji walikuwa wanatoka kambini wanaenda uwanjani, wana mawazoooo hawajui nini kitatokea.

 Hapa walikuwa katika chumba cha kubadilishia nguo, hawakukaa bure hapa walikuwa wanaangalia baadhi ya video za ruvu shooting ili kuwapa mbinu za kuwakabili... NB: Taraa mnaocheza na Coastal Under 20, wanazo video za timu zote, kocha anawaonyesha video kwanza kabla hawajaingia uwanjani, hivyo simba wajipange kesho.

                   Hapa Meneja Abdulrahman Mwinjuma 'Ubinde' akiongoza dua kabla ya mchezo.

                 Kocha wa Coastal Under 20 ndugu Shime (super coach) akipiga mafalaki kabla ya mchezo kuanza.

Vijana wakinyoosha misuli kabla ya mchezo.... makinikaaa Coastal U/20 wamejipangaaa...

 Hapa meneja Ubinde akishangilia ushindi na vijana wake ni baada ya kuisha penalt Ruvu Shooting walikosa penalt 2 katika 5 na Coastal walikosa 1 katika 5.

 Mzee Mguto makamu mwenyekiti Coastal Union nae alikuwepo, hapa akimwangalia mchezaji wake alieweka mabao mawili peke yake katika dakika 90 za kawaida na kuisha 2-2 hivyo ni kama ameipeleka timu nusu fainali. Anaitwa Mohammed Miraji au Muddy magoli....

Picha bado zipo nyingi, lakini mtandao unasumbua, kesho naahidi kuweka nyingine zaidi. Hii picha niliipiga nikiwa mbali, hapa ilikuwa Half time. Coastal wapo nyuma kwa goli 2-0. Eddy Shossi na Ubinde wakiwa wamevurugwa. Hawajui wafanye nini tayari walishakubali matokeo ila hawajui wataingia Tanga na uso gani.... Kaa nami baadae nitakuonyesha picha baada ya penalt kuisha, Mungu akajaalia wakaja eneo hilihili nikawapiga picha wakiwa wanacheeeekaaa wameshasahau kama walikaa katika eneo hili wakiwa wamenuniana.... ahahaaaa ukiwa mpiga picha raaaha kweli...

to be continued..... stay tuned..

No comments:

Post a Comment