Friday, December 21, 2012

tulipoachia jana....

 Hapa ni mapumziko kocha Shime akiwapa mbinu vijana wake na kuwaambia wale mbona weupe tu kama hizo jezi mlizovaa?

                                              Mara akaingiwa huyo mtoto wa kuitwa Messi...

 Hiki ni kipindi cha pili dakika ya thamanini Simba 1- 2 Coastal, hapa viongozi wa Simba wakiwa wamevurugwa.

                           Viongozi wa Coastal walikuwa wanacheka tu.... wanaomba mpira uishe...

 Hapa ni baada ya mpira kuisha, viongozi wakitambulishwa majembe mapya ya Coastal kubwa....

Namuona Dk wa Timu (alievaa begi mgongoni) akikatiza mbele ya camera ya jembe. Kwa mbaaali namuona Shime akimpongeza mchezaji wake.

 Unajua Godfrey Nyange 'kaburu' makamu mwenyekiti Simba SC ni mzungu? Hapa akikumbatiana na mwenyekiti wa Coastal Aurora, baada ya mechi kuisha...

                                                               Kaburu anakubali kiaina....

                                                     Mlezi wa wana Hemed Aurora na wanawe...

                          Makamu mwenyekiti Coastal Mzee Mnguto nae alikuwepo kama kawaida yake...

                                  Kocha Shime akiwa amebebwa juu juu kama Morinho vile..

 Hapa jembe nikiwa na Eddy Shossi tukionyeshwa picha maalum na mwenyekiti. Picha hiyo nitaitoa leo katika kidojembe.... nikisahau nikumbusheni.

 Huyu mwenye miwani ni mzee Bwanga,mchezaji wa zamani wa Coastal na baadae akahamia timu nyingine akizungumza na Jamhuri Kihwelu baada ya mechi kuisha. Julio anaijua vizuri Coastal...

 Dereva wa Coasta Willie akiwa na jembe pamoja na meneja Ubinde katika kambi ya coastal jana.

                                                           Ilikuwa ni nderemo na vifijo..

No comments:

Post a Comment