Sunday, December 16, 2012

Jamani Jakaya Kikwete yamemkuta mengi, chuo cha Monduli aliondoka akiwa ameacha mikasa mingi sana, ila leo amerejea kama Amiri jeshi mkuu wa chuo hicho... raaaha sio raahaaa?

 Hili ni jengo la maktaba ambalo Jakaya amelizindua jana katika harakati za kuhakikisha jeshi la wananchi Tanzania halizlishi mambumbumbu katika chuo chake.

Hili ni bweni namba 15 ambacho ndicho chumba alichokuwa akilala Kikwete alipokuwa mafunzoni chuoni Monduli. Inasemekana Rais Kikwete alisoma chuoni Monduli akafikia ngazi ya mkufunzi wa siasa, ila alikorofishana na mkuu wake chuoni hapo akafikia kukimbia ndipo TANU ikamuingiza katika ajira akawa ni mwajiriwa wa TANU. Sasa leo hii amerejea akiwa amiri jeshi mkuu ambapo aliwatunuku kamisheni maafisa192 ambao wamehitiu mafunzo yao chuoni hapo jana.

No comments:

Post a Comment