Friday, March 8, 2013

Mahakama kuu nchini Kenya kuamua ikiwa ina uwezo wa kusikiliza kesi ya uchaguzi ama la...


Siku nne baada ya kupiga kura wakenya wangali kujua mshindi, wa urais, baadhi ya yaliyojitokeza hadi sasa ni pamoja na malalamishi ya muungano wa CORD wake Raila Odinga kutaka tume ya uchaguzi kusitisha shughuli ya kuhesabu kura wakidai kufanyika udanganyifu.
Leo mashirika ya kijamii yamekwenda mahakamani kuitaka mahakama kuu kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura
Nayo tume ya uchaguzi yasema idadi kubwa ya kura zilizoharibika ilitokana na hitilafu katika mtambo wake ambao ulikuwa unaongeza idadi ya kura hizo mara nane
Hadi kufikia sasa Uhuru Kenyatta ana kura 5,004,406 Raila Odinga ana kura 4,442,923
Wakenya wakiwa katika kipindi kigumu na cha wasiwasi kwani imechukua Tume ya Uchaguzi muda wa siku nne tangu kuanza shughuli ya kuhesabu kura na bado mshindi hajajulikana.
Kumekuwa na kila aina ya matukio katika muda huo wote. Tayari mashirika ya kijamii yameitaka mahakama kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura inayofanywa na tume ya uchaguzi.Muungano wa CORD unaoongozwa na tume ya uchaguzi, umelalamika ukisema shughuli hiyo ina mizengwe na wanataka ianzishwe upya.
Tupe maoni yako kwenye ukurasa wetu wa BofyaFacebook kuhusu yanayojiri Kenya na tutauweka ujumbe wako kwenye mtandao wetu Bofyabbcswahili.com

15:40Dennis Tsunami Mbaka anasema kupitia Bofyafacebook mataraiio ya wakenya ni mengi na licha ya kuzuka mambo mengi wakati huu wa uchaguzi hususan matokeo ya uchaguzi wa urais yakisubiriwa, anachotaka ni mchakato mzima kukamilika bila tashwishi na anaitakia nchi yake mustakabali mwema

15:32 Kuhusu kesi ambayo mashirika ya kijamii yameishtaki tume ya uchaguzi na kuitaka ikomeshe shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura za urais, ni mapema mno kwa hilo. Duru za kisheria zinasema kuwa kesi hiyo ina misingi duni kwani wanapaswa kusubiri matokeo rasmi ya uchaguzi kutangazwa ndiposa waende mahakamani

15:25 Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan anatarajiwa kuhutubia waandishi wa habari wakati wowote kuanzia sasa
15:21Hanif Mohammed akiwa mjini Mombasa ameandika kwenye ukurasa Bofyafacebook akizungumzia matokeo ya uchaguzi kwa sasa ya wagombea wakuu kuwa wanakanganywa na hesabu ya kura hizi ila anachoomba tu ni kuwepo amani

15:14 Sebastian Sabato kwenye ukurasa wa Bofyafacebook anasema, ijapokuwa ninasubiri matokeo kwa hamu na gamu, kwa upande mwingine shughuli zangu zinaendelea kama kawaida.

wakati huohuo imeripotiwa kuwa:

Mahakama ya juu nchini Kenya hii leo itatoa uamuzi ikiwa ina uwezo wa kusikiliza kesi iliyowasilishwa kwake na makundi ya kijamii yakitaka tume huru ya uchaguzi nchini Kenya kusitisha shughuli ya kuhesabu kura za urais inayoendelea katika ukumbi wa Bomas.
Makundi hayo yanadai kuwa tume inakwenda kinyume na katiba ambayo ambayo inasema kura zinapaswa kuhesabiwa kwa njia ya elektroniki.
Pia Muungano wa Cord wake mmoja wa wagombea wa urais Raila Odinga umedai kuwa tume hiyo inafanya hujuma katika shughuli ya kujumlisha kura za urais katika ukumbi wa Bomas.
Hapo jana Muungano wa CORD ulielezea malalamishi kuhusu shughuli yakujumlisha kura za urais na kusema hauna imani nayo kwani ina ushahidi kuwa hujuma imefanyika wakidai wizi wa kura.
Pia wanadai kuwa katika baadhi ya maeneo, kura zilizopigwa ni nyingi kuliko idadi ya wapiga kura waliosajiliwa.
Madai haya waliyatoa hapo jana ingawa mkuu wa tume ya uchaguzi aliyakanusha vikali na kusema hakuna mahala popote ambapo wameshuhudia matokeo kuhujumiwa.
Chama hicho pia kilidai kuwa baadhi ya matokeo yalikuwa juu ikilinganishwa na idfadi ya wapiga kura.
Na kwa hilo, mkuu wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan pia alikanusha vikali akisema hawajapata matokeo kama hayo.
Tume hiyo imesisitiza kuwa shughuli ya kuyahakiki matokeo inafanywa mbele ya maajenti wa vyama vyote.
Wakati huohuo tume hiyo imekiri kuwa kulikuwa na tatizo la mtambo wake wa kupeperusha matangazo ikisema kuwa ilikuwa inaongeza mara nane kura zilizoharibika.
Washika dau wengi walieleza wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya kura zilizoonekana kuharibika kwani zilikuwa kura zaidi ya laki tatu. Lakini kufikia sasa zimepungua na kufika themanini.
Mkuu wa tume hiyo, Issack Hassan alisema kuwa komputa ilikuwa inaongeza idadi ya kura zilizoharibika kwa mara nane.
Shughuli ya kukusanya matokeo ilianza upya kwa mikono kufuatia matatizo haya lakini Uhuru Kenyatta angali anaongoza dhidi ya Raila Odinga.
"kulikuwa na makosa kwa namna ambavyo programu ya komputa ilikuwa imeundwa, '' alisema Hassan.
''Kwa kura zote zilizoharibika kwa kila mgombea zilikuwa zinaongezeka mara nane ,'' aliongeza kusema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.
Chanzo: BBC Swahili.

No comments:

Post a Comment