Uhuru Muigai Kenyatta
amezaliwa 26 Oktoba 1961 ni mwanasiasa wa Kenya ambaye amekuwa Naibu Waziri
Mkuu tangu 2008. Yeye ni Mbunge wa Jimbo Gatundu Kusini na Mwenyekiti wa zamani
wa Kenya African National Union (KANU), ambayo ilikuwa ni sehemu ya Party of
National Unity (PNU).
Kenyatta ni mtoto wa kwanza
Jomo Kenyatta, Rais wa kwanza wa Kenya (1964-1978). Alisoma shule ya St Mary Nairobi. Baadae akajiunga na
chuo cha amherst kusomea sayansi ya siasa nchini Marekani.
Alikuwa mbunge mwaka
2001, akawa Waziri wa Serikali za Mitaa chini ya Rais Daniel arap Moi na, licha
ya kukosa uzoefu wa kisiasa, ilikuwa Rais Moi alipendelea awe mrithi wake;
Kenyatta alikuwa mgombea wa KANU katika uchaguzi wa rais Desemba 2002, lakini
walishindwa na mgombea urais wa upinzani Mwai Kibaki kwa kiasi kikubwa. Hatimaye
akawa Kiongozi wa Upinzani katika Bunge.
Baadae Kenyatta
akasaidia kurejea kwa Mwai Kibaki katika nafasi ya Urais Desemba 2007 na
ikuteuliwa Waziri wa Serikali za Mitaa Januari 2008, kabla ya kuwa Naibu Waziri
Mkuu na Waziri wa Biashara Aprili 2008 kama sehemu ya serikali ya mseto.
Hatimaye Kenyatta
alikuwa Waziri wa Fedha 2009-2012, huku akiendelea kushikilia nafasi ya Naibu
Waziri Mkuu. Kutokana na mahakama ya kimatifa ya makosa ya jinai (ICC)
kumtuhumu kuwa miongoni mwa viongozi waliochochea ghasia za uchaguzi wa 2007,
Kenyatta aliamua kujiuzulu kama Waziri wa Fedha tarehe 26 Januari 2012.
Historia inaonyesha
Uhuru Kenyatta aliingia katika siasa mnamo mwaka 1997 wakati aliposhiriki
uchaguzi wa uenyekiti tawi la chama cha KANU. Ambao ulikuwa ni mpango wa Rais
Moi kumuandaa kwa uongozi baadae.
Katika uchaguzi mkuu
uliofanyika mwaka huo huo, Uhuru aligombea kiti cha ubunge jimbo la Gatundu
kusini. Kwa bahati mbaya alianguka katika uchaguzi huo, na kufikia kutaka
kuachana na masuala ya siasa.
Baada ya kuanguka
uchaguzi huo Uhuru aliamua kuelekeza nguvu zake katika bishara za familia
ambazo ni pamoja na hoteli za kitalii za nyota tano, mashirika ya ndege na
kilimo cha biashara. Bila kujua kuwa Rais Moi alikuwa bado na dhamira ya kumwingiza
katika siasa.
Mwaka 1999 Moi
alimteua Uhuru mwenyekiti mpya wa Bodi ya Utalii ya Kenya, ambako alifanya kazi
na mwanasiasa mkongwe nchini humo Nicholas Biwott, ambae ni mtu wa karibu sana
na Rais Moi. Ambapo Uhuru alipikwa vilivyo katika ulingo wa siasa kwa kuwa
karibu na Biwott.
Ndipo Oktoba 2001 Uhuru
alikuwa mbunge wa kuteuliwa na kuingizwa katika baraza la mawaziri kama Waziri
wa Serikali za Mitaa. Katika Machi mwaka huu Uhuru Kenyatta alifanya hivyo
kubwa katika mazingira ya siasa akachaguliwa kama moja ya nne ya kitaifa makamu
wenyeviti wa KANU.
Rais Moi alitaka kuhakikisha
Kenyatta alikuwa mgombea urais wa KANU, na takwimu inaonyesha Uhuru aliamua
kupambana na nafsi yake ili asimame mwenyewe na asionekane ni kibaraka wa Moi.
Ndipo mwishoni mwa
Januari 2005, Uhuru Kenyatta alimshinda Nicholas Biwott katika kinyanganyiro
cha uenyekiti wa KANU, alishinda kwa kura 2,980 kati ya wajumbe wa chama dhidi
ya 622 za Biwott.
Chini ya uongozi wa
Uhuru kama waziri wa fedha alianzisha mpango maalum wa kuchochea ukuaji wa
uchumi nchini Kenya. Lengo likiwa ni kuchochea shughuli za uchumi nchini humo,
fursa za ajira, kuhimiza uvumbuzi katika kukuza utajiri, kuchochea ujasiriamali
na kusaidia sekta ya afya, elimu na ubunifu.
Hata hivyo, tarehe 15
Desemba 2010, Kenyatta Uhuru alitajwa kama mtuhumiwa wa uhalifu wa kimataifa
dhidi ya binadamu chini ya mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya
makosa ya jinai (ICC) Moreno Ocampo, kwa ajili ya kupanga na kufadhili ghasia
katika mji wa Naivasha na Nakuru.
Kura bado zinaendelea kuhesabiwa.
Ingawa Uhuru hapo
awali alikanusha wito wa (ICC), hatimae aliamua kuheshimu wito wa kuenda
mahakamani yeye na mkuu wa utumishi Balozi Francis Muthaura na kamishna wa
Polisi Hussein Ali. Lengo ni kutaka
kujua kama watakuwa na kesi ya kujibu ama la, lakini mnamo tarehe 23 Januari
2012, ICC alithibitisha kesi dhidi ya Kenyatta na Muthaura.
HAFIDH KIDO
kidojembe@gmail.com
5 March, 2013
Dar es Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment