Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya imekiri kuwa
kulikuwa na hitilafu chungu nzima za kimitambo, katika kutoa matangazo ya
matokeo ya kura za urais kutoka kwa vituo vya kupigia kura kote nchini.
Afisaa mkuu mtendaji wa tume hiyo,James Oswago alielezea kuwa
hitilafu hiyo ilisababishwa na kiasi kikubwa cha matokeo yaliyokuwa
yanapeperushwa moja kwa moja kutoka kwa vituo vya kupigia kura kwa sababu ya
ukosefu wa nafasi ya kutosha kwenye mitambo yake.
Akihutubia waandishi wa habari katika ukumbi
wa Bomas ambako matokeo ya urais yanatarajiwa kutangazwa, Bwana oswago alisema
kuwa tume hiyo iliweza kurekebisha mitambo yake.
Pia
aliongeza kuwa maajenti wa wagombea wote wakuu wawili walifahamishwa kuhusu
hutilafu hiyo.
Kugoma
kwa muda kwa mitambo ya kupeperusha matokeo, ilisababisha hali ya wasiwasi,
baada ya IEBC kusitisha kupeperusha matangazo kwa masaa kadhaa.
Maafisa
wa Miungano yote ya Jubiliee na CORD, walitetea kwa sababu ya kucheleweshwa kwa
matokeo na kulaumu tume ya IEBC, baada ya maafisa wake wote kuondoka katika
ukumbi wa kutangazia matokeo ya urais.
Kamishna
mmoja mkuu wa tume hiyo aliwataka watu kuwa watulivu akisema hakuna sababu ya
watu kuwa na wasiwasi.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment